Lambo

Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani.

Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake.

Lambo
Lambo la Aswan kwenye Ziwa la Nasser katika Misri
Lambo
Ukuta wa lambo

Shabaha ya kujenga lambo

Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.

Lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.

Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili iko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.

Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.

Shida za malambo

Kuna pia matatizo ya malambo:

  • Ukuta unaathiri uwiano wa ekolojia; kwa mfano lambo la Aswan linazuia matope yenye rutuba yasifikie Misri
  • Umwagiliaji katika nchi za joto unaweza kuharibu ardhi ukiiongezea chumvi kwa njia ya uvukizaji
  • Mara nyingi wenyeji wamefukuzwa katika eneo la ziwa jipya bila kupewa makazi mazuri
  • Penye hatari ya tetemeko la ardhi uzani wa maji umeongeza matetemeko
  • Lambo linaweza kusababisha ajali na hata maafa likipasuka na kiasi kikubwa cha maji kilichozuiliwa na ukuta wake kushuka ghafla na kuharibu makazi ya watu, mashamba na miundombinu kwenye njia yake.

Malambo makubwa ya Afrika

Picha za malambo

Marejeo

Viungo vya nje

Lambo 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


Lambo  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Tags:

Lambo Shabaha ya kujenga lamboLambo Shida za malamboLambo Malambo makubwa ya AfrikaLambo Picha za malamboLambo MarejeoLambo Viungo vya njeLamboMajiMtoMvuaUkuta

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ukanda wa GazaSayariHarmonizeMazingiraOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMkoa wa IringaVipera vya semiShambaMgonjwaTashbihaVidonge vya majiraKontuaPemba (kisiwa)Injili ya MathayoViwakilishi vya urejeshiUkristoUandishi wa barua ya simuMikoa ya TanzaniaMoyoMafurikoAla ya muzikiSerie AUenezi wa KiswahiliUfeministiItikadiAkiliUbunifuNyangumiMaajabu ya duniaBiblia ya KikristoUfinyanziUfugaji wa kukuDhamiraZuchuMamba (mnyama)Muziki wa hip hopTungo kishaziMoses KulolaVieleziMwenge wa UhuruViwakilishi vya pekeeKenyaPasakaTahajiaMofimuWasukumaHadhiraViwakilishi vya kuulizaKinywajiJipuToharaVipaji vya Roho MtakatifuNandyMkoa wa Unguja Mjini MagharibiMbuniFalsafaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaNahauMkoa wa Dar es SalaamUsawa (hisabati)WapogoloMuungano wa Tanganyika na ZanzibarJinaUtandawaziWamasoniUharibifu wa mazingiraNyegereLigi Kuu Uingereza (EPL)Haki za watotoSentensiMadhara ya kuvuta sigaraAjuzaLingua frankaTanganyika African National UnionWabena (Tanzania)🡆 More