Alhamisi: Moja ya siku saba za wiki

Alhamisi ni siku ya tano katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo.

Iko kati ya siku za Jumatano na Ijumaa. Katika hesabu ya kimataifa ya ISO 8601 ni siku ya nne.

Wikendi katika nchi za Kiislamu

Nchi kadhaa za Waislamu huanza mapumziko ya wikendi kwenye Alhamisi kama Ijumaa ni siku ya mapumziko. Hii si nchi zote za Kiislamu. Kwa mfano Misri wafanyakazi huanza wikendi Alhamisi na kuendelea Ijumaa; Uturuki inatumia wikendi ya magharibi yaani Jumamosi-Jumapili.

Siku ya tano au siku ya nne?

Katika muundo wa juma wa kibiblia Alhamisi ni siku ya tano. Kanuni ya ISO 8601 ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hivyo Alhamisi ni namba 4. Jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea hesabu ya kale.

Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali

Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "5" ndani yake lakini haieleweki kirahisi kwa sababu Alhamisi ina asili ya lugha ya Kiarabu. خميس (khamis) ni namba tano tu. Kiswahili chenyewe chatumia namba hii katika jina la siku ya Jumatano inayotangulia Alhamisi. Pamoja na Ijumaa ni siku ya pekee yenye jina la Kiarabu katika lugha ya Kiswahili.

Majina ya siku zingine yameanzishwa upya katika Kiswahili kuanzia siku ya sala ya pamoja ya Waislamu kwenye Ijumaa kuzitaja kama Juma-mosi, Juma-pili n.k.

Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuita siku hiyo kwa namba "tano". Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita "siku ya tano", kwa mfano Kiindonesia (Kamis - ya tano) au Kiajemi (Farsi) (پنج‌شنبه - panch shanbe - siku ya tano).

Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Jeudi" (siku ya Jovi au Jupiter) au Kiingereza "Thursday" (siku ya Thor).

Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi

Tags:

ISO 8601IjumaaJumaJumatanoUkristoUyahudi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

John Raphael BoccoMoshi (mji)PunyetoMlima wa MezaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniWairaqwMafua ya kawaidaFalme za KiarabuFigoMpwaDar es SalaamJumuiya ya MadolaMkoa wa KilimanjaroSteve MweusiMaigizoAli Hassan MwinyiYouTubeRwandaHistoria ya KenyaInjili ya LukaMkoa wa MbeyaAlomofuUtoaji mimbaTafsidaNomino za wingiHedhiAla ya muzikiChuo Kikuu cha PwaniAlgorithimu uchanguajiMaambukizi nyemeleziNuktambiliMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMtemi MiramboMichezo ya watotoNangaWaziri Mkuu wa TanzaniaMatiniMbossoAfro-Shirazi PartyBiashara ya watumwaMkoa wa KataviUkimwiHistoria ya uandishi wa QuraniHerufiAina za ufahamuSikioHifadhi ya Taifa ya NyerereBabeliLatitudoMkonoMickey MouseVita Kuu ya Kwanza ya DuniaDodoma (mji)SerikaliRamaniOrodha ya Magavana wa TanganyikaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaVitenzi vishiriki vipungufuMeena AllyUandishi wa ripotiMkoa wa TangaSamia Suluhu HassanMziziLugha za KibantuHoma ya matumboVita vya KageraHurafaBiblia ya Kikristo🡆 More