Walarasi

Nususpishi 3:

Walarasi
Walarasi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Odobenidae (Wanyama walio na mnasaba na walarasi)
Jenasi: Odobenus
Brisson, 1762
Spishi: Odobenus rosmarus
(Linnaeus, 1758)
Ngazi za chini

  • O. r. divergens (Illiger, 1815)
  • O. r. laptevi Chapskii, 1940
  • O. r. rosmarus (Linnaeus, 1758)
Msambao wa walarasi (zambarau)
Msambao wa walarasi (zambarau)

Walarasi (kutoka Kiing.: walrus, pia huitwa nguva aktiki au sili-pembe; Kisayansi: Odobenus rosmarus) ni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva wa kawaida mwenye meno mawili marefu, yanayoitwa pembe pia, kama tembo.

Etimolojia

Neno la "walarasi" linatoka neno la Kiingereza "walrus" litokalo labda maneno ya Kiholanzi "walvis" (nyangumi) na "ros" (farasi) lakini inawezekana zaidi kwamba walrus linatoka neno la Kinorwei cha Kale "hrossvalr". Jina la "nguva aktiki" linatoka neno la nguva kwa sababu mara nyingi mnyama huyu amechanganyikwa na nguva halisi. Huitwa "sili-pembe" kwa sababu mnyama huyu ana mnasaba na sili (wako pamoja katika kundi la kitaksonomia la Pinnipedia).

Anatomia

Vifuko vya hewa chini ya koo shingoni mwa walarasi, shingo lililo fupi na nene, vifuko hivyo vina uwezo wa kuvimba na hewa ili kumpa uwezo wa kuelea wima na kichwa chake juu ya maji. Pia vinatumiwa kama vyumba vya mvumo vinavyotoa sauti kama kengele chini ya maji. Kinyume ya vikono vya nyuma, haya ni marefu kama yaliyo mapana, lakini yana unene na gegedu na vidole vitano kama vikono vya nyuma. Wanapoogelea, yanatumiwa mara kwa mara kupiga kasia katika mwendo ulio chini lakini mara nyingine hutumiwa kuelekeza. Masikio yao madogo yana kunyanzi ya ngozi nje yao ili kufanya vichwa vyao vinyooke ili waogelee vyema zaidi majini. Walarasi ni mdogo kuliko tembo-bahari aliye mkubwa kabisa kati ya Pinnipedia (wanyama wenye miguu-mapezi).

Pembe

Zimeundwa na dentini, pembe za walarasi ni ndefu sana na ni meno yanayoendelea kukua. Hazitumiwi kuchimbia chakula lakini huwapea usaidizi mwingi wanapojikokota barafuni au ardhini. Pia zinatumiwa kuonyesha utawala na cheo.

Ngozi

Ngozi ni ya hudhurungi yenye kunyanzi inayoonekana kama inabadilisha rangi kulingana na halijoto, kwa sababu wakati anapohisi joto, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi huongezeka ili kumpoza. Tendo hili humpatia walarasi sura nyekundunyekundu na huonekana kama ana madoadoa. Anapohisi baridi, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi hupunguzika, kumpatia sura ya kukwajuka. Tabaka ya shahamu kubwa iliyo na upana wa hadi sentimita 15 inayomkinga kutoka kwa baridi.

Sharubu

Sharubu zao zilizo puani ni nene na zina hali ya juu ya kuhisi na husaidia wanapotafuta chakula.

Utalii

Walarasi  Makala hii kuhusu "Walarasi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili nguva, sili kutoka lugha ya Kiswahili. Neno (au maneno) la jaribio ni nguva aktiki, sili-pembe.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Walarasi  Makala hii kuhusu "Walarasi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili walrus kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni walarasi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Tags:

Walarasi EtimolojiaWalarasi AnatomiaWalarasi UtaliiWalarasi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

NuktambiliTenzi tatu za kaleMkoa wa SongweInstagramBenderaHistoria ya Kanisa KatolikiJuxMadiniUundaji wa manenoHifadhi ya SerengetiKiarabuKongoshoInshaUlimwenguMagharibiLuhaga Joelson MpinaEdward SokoineJay MelodyMsamiatiKata za Mkoa wa MorogoroUandishiNgonjeraAfrika ya MasharikiUmaskiniUtendi wa Fumo LiyongoMillard AyoKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniSwalaBahari ya HindiMwakaLiverpoolNahauUingerezaMkoa wa RuvumaMichezoMitume wa YesuMbogaJamiiNomino za wingiMohamed HusseinFamiliaDaudi (Biblia)Jakaya KikweteLongitudoDhima ya fasihi katika maishaMshororoJamhuri ya Watu wa ZanzibarKomaMzeituniMmeaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMafumbo (semi)Orodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaTamthiliaMkuu wa wilayaDubaiTupac ShakurMusaSimbaBaraWilaya ya IlalaNembo ya TanzaniaManchester CityMsituFonolojiaRayvannyHistoria ya IranKaswendeMvuaMaudhui katika kazi ya kifasihiBabeliMadhara ya kuvuta sigara🡆 More