Trinidad Na Tobago

Jamhuri ya Trinidad na Tobago ni nchi ya visiwani katika Karibi ya kusini, karibu na pwani ya Venezuela, kusini kwa kisiwa cha Grenada cha Antili Ndogo.

Nchi jirani nyingine kuvukia bahari ni Barbados na Guyana.

Trinidad na Tobago

Nchi ina eneo la km² 5,128 ambalo karibu lote ni kisiwa kikuu cha Trinidad. Kile cha Tobago kina asilimia 6 tu za eneo pamoja na 4% ya wakazi. Kuna visiwa vidogo vingine 21.

Ni jamhuri mwanachama wa Jumuiya ya Madola.

Ni nchi iliyoendelea, ikishika nafasi ya tatu kati ya zile za Amerika baada ya Marekani na Kanada.

Historia

Visiwa vilikaliwa na Waindio kwa karne nyingi kabla ya ujio wa Kristofa Columbus na Wahispania (1498).

Trinidad ilibaki chini ya wakoloni hao hadi mwaka 1797 vilipotekwa na Waingereza ambao walikabidhiwa pia Tobago mwaka 1802. Viliunganishwa mwaka 1889 na kubaki koloni hadi mwaka 1962 vilipopata uhuru.

Mwaka 1976 nchi imeanza kuwa jamhuri.

Watu

Wakazi wengi wana asili ya India (37.6%), lakini pia ya Afrika (36.3%) na sehemu nyingine. Hivyo kuna machotara wa aina mbalimbali (24.2%).

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wananchi wengi wanaongea kwa kawaida aina mbili za Krioli. Asilimia 5 wanaongea Kihispania.

Upande wa dini wengi (63%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (21.5%), Wapentekoste (12%) na Anglikana (5.7%). Wahindu ni 18% na Waislamu ni 5%.

Tazama pia

Viungo vya nje

Trinidad Na Tobago 
WikiMedia Commons
Trinidad Na Tobago  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Trinidad na Tobago kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Trinidad Na Tobago HistoriaTrinidad Na Tobago WatuTrinidad Na Tobago Tazama piaTrinidad Na Tobago Viungo vya njeTrinidad Na TobagoAntili NdogoBahariBarbadosGrenadaGuyanaKaribiKisiwaKusiniNchi ya visiwaniPwaniVenezuela

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MadinaLionel MessiMvuaRobin WilliamsVivumishi vya pekeeUbatizoZuhura YunusKitubioAsili ya KiswahiliKifo cha YesuSiasaVipera vya semiAustraliaUshogaMamlaka ya Mapato ya TanzaniaMkoa wa KigomaLughaUzazi wa mpango kwa njia asiliaMakabila ya IsraeliKata za Mkoa wa Dar es SalaamWamasaiJustin BieberMwenyekitiFisiVita Kuu ya Pili ya DuniaLilithMkoa wa IringaOrodha ya Magavana wa TanganyikaMalariaVivumishi vya sifaDiniOrodha ya Marais wa TanzaniaRené DescartesJamhuri ya Watu wa ZanzibarUfufuko wa YesuTungo kishaziChadChatuMkoa wa MaraMkoa wa NjombeUpinde wa mvuaMungu ibariki AfrikaMafua ya kawaidaJohn Raphael BoccoIdi AminElimuSalamu MariaAsiaVieleziAntibiotikiHadithiWairaqwRedioMgawanyo wa AfrikaGesi asiliaNetiboliKamusiWazaramoMtiWikimaniaMaajabu ya duniaAnna MakindaKumaNabii EliyaHoma ya manjanoAngkor WatWema SepetuMbuniDizasta VinaKorea KusiniMitume na Manabii katika UislamuMshororoUchimbaji wa madini nchini TanzaniaWikipediaMuda sanifu wa dunia🡆 More