Skype

Skype (matamshi: / skaɪp /) ni programu ambayo inatumia intaneti kupiga simu za sauti na video kwa teknolojia inayoitwa Voice over Internet Protocol (VoIP).

Skype huwezesha watumiaji kutuma ujumbe wa maneno, video, sauti, picha na kufanya mikutano kwa video.

Nembo ya Skype
Nembo ya Skype

Iliundwa mwaka 2003 na Mswidi na Mdenmark Niklas Zennström na Janus Friis wakishirikiana na Waestonia Ahti Heinla, Priit Kasesalu, na Jaan Tallinn, na kwa sasa inaendeshwa na kampuni ya huko Luxemburg inayoitwa Skype Technologies SARL, ambayo tangu mwaka k2011 ni sehemu ya Microsoft.

Kabla ya kumilikiwa na Microsoft, Skype ilimilikiwa na eBay kuanzia Septemba 2005 hadi 2011. eBay iliinunua kutoka kwa walioizindua kwa dola za Kimarekani bilioni 2.6 miaka 2 baada ya kuzinduliwa.

Mwaka wa 2009, eBay iliuzia Silver Lake, Andreessen Horowitz, na Bodi la Mipango ya Uwekezaji wa Pensheni la Kanada asilimia 65 ya hisa za Skype kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 1.9 wakati thamani ya Skype ilikuwa takriban dola za Kimarekani 2.75.

Tarehe 10 Mei 2011, Microsoft ilianza mipango ya kumiliki Skype Communications, S.à r.l kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 8.5 na tarehe 13 Oktoba mwaka huo mipango ya umiliki ikakamilika.

Jina Skype linatokana na "Sky peer-to-peer" ambapo ilifupishwa kuwa "Skyper". Hata hivyo, anuani ya tovuti yenye jina hilo ilikuwa tayari imenunuliwa na kampuni nyingine, hivyo herufu "r" iliondolewa na kuwa Skype.

Marejeo

Viungo vya nje

Skype  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Skype kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

IntanetiMatamshiNenoPichaProgramuSautiSimuTeknolojiaUjumbeVideo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jakaya KikweteUharibifu wa mazingiraJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoHomoniDiglosiaKitenzi kishirikishiPapa (samaki)UchawiAgostino wa HippoKiambishiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoDini asilia za KiafrikaUbadilishaji msimboHerufiYoung Africans S.C.UjerumaniEe Mungu Nguvu YetuMaudhui katika kazi ya kifasihiMfumo wa Msimbo wa Posta TanzaniaMperaMkoa wa ArushaIkwetaBenjamin MkapaRiwayaOrodha ya Magavana wa TanganyikaUenezi wa KiswahiliHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoRedioMsokoto wa watoto wachangaNgamiaMkopo (fedha)MasharikiLigi Kuu Uingereza (EPL)Kimara (Ubungo)Wayback MachineMtume PetroKenyaUvimbe wa sikioTanzaniaMimba kuharibikaUzalendoMkunduUmoja wa AfrikaHurafaVisakaleMwanamkeSerikaliAfrika ya MasharikiSaidi NtibazonkizaMbagalaJava (lugha ya programu)TarakilishiUkristoAfrikaMapambano ya uhuru TanganyikaKumaKiwakilishi nafsiP. FunkSheriaAgano JipyaTashihisiHarmonizeUsawa (hisabati)Utumbo mpanaSinagogiOrodha ya majimbo ya MarekaniHadhiraMaishaOrodha ya kampuni za TanzaniaTafakuriTupac ShakurMkoa wa LindiKoma🡆 More