Mashapo

Mashapo (kwa Kiingereza: sediment) ni vipande vidogo vya mata thabiti vilivyovunjika na nguvu za maji, barafu, upepo, kwa njia ya mmomonyoko na mabadiliko ya halijoto, halafu kusafirishwa na maji, barafu, upepo au mvuto wa graviti.

Mashapo
Mto wa mlimani husafirisha hata mawe makubwa katika mashapo yake.
Mashapo
Milia katika jiwe mchanga inaonyesha jinsi mashapo yalivyobaki moja juu ya mengine katika mwendo wa mamilioni ya miaka na kuwa mwamba mashapo baadaye.

Vipande hivyo vilivyovunjika hutokea kama matope, mchanga na mawe. Vikisafirishwa na maji ya mto vinabaki chini baadaye, wakati nguvu ya maji inapungua. Sehemu kubwa inafika baharini; kiasi cha mashapo yote kutoka mito yanayoishia baharini ni vigumu kukitaja kwa uhakika, kiliwahi kukadiriwa kuwa tani 13.5-15 x 10 (tani bilioni 15)9 hadi tani bilioni 20 kwa mwaka.

Hasa katika maeneo ya mafuriko ya kujirudia mashapo yaliyobaki hufunikwa tena na mashapo mapya ambayo kwa njia hiyo yanaweza kujenga matabaka manene ya ardhi au ya mawe. Katika muda wa milioni za miaka matabaka hayo ya mashapo yanaweza kubadilishwa kuwa mwamba mashapo.

Mashapo ya matope matupu yanaweza kuunda ardhi nzuri ya mashamba, au udongo wa mfinyanzi unaoweza kuendelea kubadilika kuwa mwambatope kama grife. Mashapo ya mchanga husababisha kutokea kwa ufuko wa mchanga baharini, au matabaka ya mchanga yanayochimbwa kwa mahitaji ya ujenzi. Vivyo hivyo kokoto na mawe madogo ambayo mara kwa mara yanapatikana kwa wingi katika sehemu zilizokuwa zamani njia za mito.

Tanbihi

Marejeo

  •  
  •  
  •  
  •  
Mashapo  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mashapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BarafuGravitiHalijotoKiingerezaMajiMataMmomonyokoNguvuUpepo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Simu za mikononiFalsafaUgandaHistoria ya Kanisa KatolikiArusha (mji)Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Wilaya ya TemekeMbagalaKitenziKitenzi kikuu kisaidiziVivumishiMkoa wa SimiyuUaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaUnyenyekevuHurafaAfrika ya MasharikiVidonda vya tumboAndalio la somoSitiariJichoAfrika Mashariki 1800-1845IfakaraWilaya ya NyamaganaKitenzi kishirikishiMandhariBungeHifadhi ya SerengetiViwakilishi vya urejeshiMtakatifu PauloYesuMtumbwiBendera ya KenyaLeonard MbotelaWagogoOrodha ya makabila ya TanzaniaRita wa CasciaSabatoUkristo nchini TanzaniaMsamahaKisaweUkristoUtendi wa Fumo LiyongoEl NinyoDoto Mashaka BitekoKiarabuMohamed HusseinUbongoP. FunkKarafuuUDAWilayaChuo Kikuu cha Dar es SalaamOrodha ya Marais wa KenyaIndonesiaVitenzi vishirikishi vikamilifuUkooNominoTambikoKhadija KopaJakaya KikweteMsokoto wa watoto wachangaMkoa wa MwanzaBidiiDalufnin (kundinyota)Majigambo25 ApriliHuduma ya kwanzaLahaja za KiswahiliUundaji wa manenoNenoTreni🡆 More