Mwamba Mashapo

Miamba mashapo (kwa Kiingereza: sedimentary rocks) hutokea pale ambapo mashapo hukaa kwa muda mrefu yakifunikwa na mashapo mengine na kuathiriwa na uzito wa matabaka ya juu yanayosababisha shinikizo kubwa.

Miamba ya aina hiyo hufanya sehemu kubwa ya uso wa ardhi, ingawa Dunia kwa jumla kuna zaidi miamba ya mgando (igneous rocks) na miamba metamofia (metamorphic rocks).

Mwamba Mashapo
Aina mbili za mwamba mashapo: chini mwambatope, juu gange. Plateau Plateau, Tennessee, Marekani.
Mwamba Mashapo
Jiwe mchanga jekundu linaonyesha tabaka jinsi mchanga wake ulivyokaa.
Mwamba Mashapo
Kuunganishwa kwa punje za mchanga zikiathiriwa na shinikizo kubwa sana. Pale punje zinapogusana shinikizo kuu linasababisha kuyeyuka kwa mata inayoanza kujaza nafasi kati ya punje. Punje zilizogusana zinaunganishwa kwa njia hii na nafasi zinapungua. Kadri shinikizo linaendelea kwa muda mrefu, mwaba huwa mgumu zaidi na kuongeza densiti. Kwa njia hii mchanga unaweza kubadilika kuwa jiwe mchanga.

Asili ya miamba mashapo

Mashapo kwa kawaida ni mata inayokusanyika chini kwenye mito, maziwa na bahari baada ya kupelekwa huko na mwendo wa maji, kiasi pia kwa mwendo wa upepo. Mata ya mashapo ni pamoja na vipande vidogo vya mawe yaliyosagwa au kuvunjikavuunjika, mabaki ya mimea au wanyama na mata yaliyotokana na utendanaji wa kikemia.

Aina za miamba mashapo

Miamba mashapo inapatikana hasa ya aina tatu: gange (mawe ya chokaa, limestone), jiwe mchanga (sandstone) na mwambatope (shale).

Miamba mashapo hufunika asilimia 75  – 80 za uso wa ardhi, lakini hufanya 5% tu za ganda la Dunia. Viwango husianifu wa aina za miamba mashapo ni kama ifuatavyo:

  • Mwambatope ---------- 60%
  • Jiwe la mchanga-- 20%
  • Gange (CaCO3) --- 15%
  • Mengine ----- 5%

Kuimarishwa

Kama mashapo yameshinikizwa kwa nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, huimarishwa na kugeuka kuwa mwamba thabiti. Iliyopandwa na kushinikizwa kwa muda, matope huwa 'yameunganishwa' (yamefanywa kuwa thabiti) kuwa safu ya mwamba. Katika mwamba huo matabaka yanatambulika yanayoonyesha jinsi gani mashapo yalivyojipanga wakati wa kushuka kwenye tako la bahari na kufunikwa na matabaka mapya.

Tanbihi

Viungo vya Nje

Mwamba Mashapo 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Mwamba Mashapo  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwamba mashapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Mwamba Mashapo Asili ya miamba mashapoMwamba Mashapo Aina za miamba mashapoMwamba Mashapo KuimarishwaMwamba Mashapo TanbihiMwamba Mashapo Viungo vya NjeMwamba MashapoDuniaKiingerezaMashapoMiamba ya mgandoMudaMwamba metamofiaShinikizoTabakaUzito

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Wayback MachineWenguDiniVirusi vya UKIMWIMfumo katika sokaChelsea F.C.Kiini cha atomuHistoria ya IsraelMazingiraLilithUpendoHaitiRadiFasihi simuliziKito (madini)PasakaDaudi (Biblia)PunyetoAdolf HitlerVihisishiAmri KumiShikamooHaki za binadamuAfrika ya MasharikiXXMtandao wa kompyutaMkoa wa MbeyaOrodha ya Magavana wa TanganyikaKiunzi cha mifupaKunguniKalenda ya GregoriDar es SalaamTajikistanAfrika KusiniDioksidi kaboniaSiasaVita Kuu ya Pili ya DuniaMtende (mti)MasharikiLeopold II wa UbelgijiJulius NyerereUenezi wa KiswahiliMziziVidonge vya majiraJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUtamaduniKalendaUmaBabeliWimboShereheInshaVichekeshoMaana ya maishaAslay Isihaka NassoroBikiraMamba (mnyama)MshororoKima (mnyama)Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoOrodha ya Marais wa MarekaniHekaya za AbunuwasiKiboko (mnyama)Kamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniLucky DubeMzabibuKupatwa kwa JuaAnna MakindaKhadija KopaMichael JacksonCAFMkoa wa KigomaVidonda vya tumbo🡆 More