Majusi

Majusi (Kiing.

magus, magi) ni mtaalamu wa nyota katika fani ya unajimu.

Majusi
Mamajusi walivyochorwa huko Ravenna (Italia), katika Basilika la Sant'Apollinare in Classe, mwaka 600 hivi.

Historia ya neno

Neno la Kiswahili limetokana na Kiarabu مجوس majus lililopokewa kutoka Kiajemi cha kale magâunô kupitia Kigiriki μάγος magos.

Kwa kuwa mara nyingi jina hilo linatumika katika wingi, linatokea ma-majusi; baadhi ya watu wakisikia au kusoma mwanzoni mwa neno silabi dabo ma-ma wanakuja kudhani ni wanawake, kumbe sivyo.

Kwa asili lilimaanisha makuhani wa dini ya Uajemi ya Kale, hasa wafuasi wa Zoroaster.

Wagiriki waliamini ya kwamba makuhani hao walikuwa na elimu ya siri hasa kuhusu nyota na utabiri wa nyota.

Kwa hiyo katika lugha kadhaa neno limeendelea kumaanisha ama wanajimu au watu waliojua maarifa ya ushirikina.

Matumizi yake ya kawaida leo

Leo kwa kawaida jina hilo linatumika kuwataja watu wa namna hiyo ambao kadiri ya Injili ya Mathayo (2:1-12) walitokea mashariki kwa Israeli wakifuata nyota ya pekee ili kumfikia Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa, yaani Yesu.

Walipofika Yerusalemu kwenye ikulu ya Herode Mkuu walimfanya afadhaike kwa habari hiyo, lakini walielekezwa Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.

Walifika na kumkuta mtoto Yesu akiwa na mama yake, Bikira Maria, wakamtolea zawadi: dhahabu, ubani na manemane.

Halafu wakaonywa wasimrudie Herode, bali warudi kwao kwa njia nyingine.

Kumbe Herode, alipoona hawarudi, akikusudia kumuua mtoto, aliagiza wauawe watoto wote wa kiume wenye umri chini ya miaka 2 katika eneo la Bethlehemu.

Liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo inakumbuka ujio wa mamajusi kwa Yesu kama mwanzo wa maandamano ya watu wa mataifa wanaokuja kumuabudu.

Sikukuu husika inaitwa Epifania, yaani Tokeo (la Bwana kwa...).

Pia kuna sikukuu yao wenyewe, tarehe 24 Julai.

Tanbihi

Majusi  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majusi kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

FaniMtaalamuNyotaUnajimu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

VihisishiMawasilianoLafudhiAbrahamuMwanza (mji)NdiziShambaBiashara ya watumwaSilabiHoma ya matumboMkoa wa MbeyaTetekuwangaWaziriShengRejistaMapenziUjerumaniAlizetiKilimanjaro (volkeno)TabataUrusiJacob StephenMafurikoUgandaKarafuuUpepoJohn MagufuliVirusi vya UKIMWIChumba cha Mtoano (2010)Clatous ChamaIntanetiUkatiliMbossoOrodha ya milima mirefu dunianiVitenzi vishiriki vipungufuAfrikaGongolambotoKonsonantiMnururishoKonyagiDubaiLugha ya taifaTanganyika African National UnionHadhiraKishazi tegemeziAthari za muda mrefu za pombeMkoa wa LindiUshairiMajeshi ya Ulinzi ya KenyaSabatoKiingerezaBurundiMarekaniLady Jay DeeUmoja wa MataifaSimba (kundinyota)Nomino za pekeeKipindupinduFananiKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniWilaya ya IlalaNamba tasaUandishi wa barua ya simuBahari ya HindiHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWilaya ya KinondoniNyangumiBunge la TanzaniaNdovuNetiboliUchumiMnyoo-matumbo MkubwaSex🡆 More