Kampuni Amazon: Kampuni ya Teknolojia ya Marekani

Amazon.com, Inc.

Kampuni Amazon: Kampuni tanzu, Marejeo, Viungo vya nje
Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos mwaka 2016.

Kampuni hiyo ndiyo kampuni kubwa kabisa duniani ya uuzaji wa bidhaa kwenye intaneti. Kwa kipimo cha mapato na mtaji wa soko, na ni ya pili baada ya Alibaba Group kwa jumla ya mauzo.

Tovuti ya amazon.com ilianza kama duka la vitabu mtandaoni na baadaye ilianza kuuza video, muziki, michezo ya video, nguo, samani, vyakula, vito n.k.

Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya kuchapisha, Amazon Publishing, studio ya filamu na televisheni, Amazon Studios, inatengeneza bidhaa za elektroniki kama vile Kindle, Echo n.k.

Amazon ina maduka ya rejareja katika nchi za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Canada, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi, Australia, Brazili, Japan, China, India, Mexico, Singapore na Uturuki.

Mnamo mwaka 2015, Amazon iliipita kampuni ya Walmart kama kampuni ya uuzaji wa rejareja yenye thamani kubwa zaidi nchini Marekani. Amazon ni kampuni ya pili ya thamani zaidi duniani (nyuma ya Apple tu), kampuni kubwa ya intaneti kwa mapato duniani, na baada ya Walmart, mwajiri wa pili mkubwa nchini Marekani.

Mwaka wa 2017, Amazon ilinunua Whole Foods Market kwa $ bilioni 13.4. Mnamo Septemba 4, 2018, Amazon ilikuwa na thamani ya dola za Marekani trilioni 1.

Kampuni tanzu

Amazon inamiliki zaidi ya kampuni tanzu 40, ikiwa ni pamoja na Zappos, Shopbop, Diapers.com, Kiva Systems (sasa inaitwa Amazon Robotics), Audible, Goodreads, Teachstreet na IMDb.

A9.com

A9.com ni kampuni inayojihusisha na utafiti na teknolojia tangu mwaka 2003.

Amazon Maritime

Amazon Maritime, Inc. ni kampuni inayomiliki meli zinazosafirisha bidhaa za Amazon toka China hadi Marekani.


Amazon Translate

Amazon Translate ni kampuni inayotumia teknolojia ya mashine ya kutafsiri.

Audible.com

Audible.com ni kampuni inayouza bidhaa za burudani ya masikioni kama vile vitabu, vipindi vya televisheni, n.k. Amazon iliinunua kampuni hii kwa dola za Kimarekani milioni $300.

Beijing Century Joyo Courier Services

Brilliance Audio

ComiXology

CreateSpace

CreateSpace ni kampuni inayotoa huduma kwa waandishi, wachapishaji, watengeneza filamu na kampuni za muziki. Kampuni hii ilikuwa kampuni tanzu ya Amazon mwaka 2009.

Goodreads

Lab126

Shelfari

Twitch

Whole Foods Market

Whole Foods Market ni kampuni inayouza vyakula visivyo na kemikali zenye kuleta madhara kwa binadamu.

Junglee

Marejeo

Viungo vya nje

Kampuni Amazon: Kampuni tanzu, Marejeo, Viungo vya nje  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amazon (kampuni) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kampuni Amazon Kampuni tanzuKampuni Amazon MarejeoKampuni Amazon Viungo vya njeKampuni Amazon19945 JulaiBiasharaJeff BezosKampuniMakao makuuMarekaniSeattleTareheWashington

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Leonard MbotelaAmri KumiOrodha ya Watakatifu WakristoHistoria ya ZanzibarJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaEe Mungu Nguvu YetuJumuiya ya MadolaMahindiAzimio la ArushaKanga (ndege)Orodha ya vyama vya siasa TanzaniaSanaa za maoneshoOrodha ya majimbo ya MarekaniYanga PrincessUsawa (hisabati)Ziwa ViktoriaAgano la KalePalestinaRupiaSensaUkabailaUingerezaPombeUtumbo mpanaChuo Kikuu cha Dar es SalaamPasakaVasco da GamaSanaaOrodha ya nchi za AfrikaPichaKukiHadhiraStephane Aziz KiHistoria ya uandishi wa QuraniBenderaShukuru KawambwaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMajiVitenzi vishiriki vipungufuBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiInstagramSoko la watumwaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaSimba (kundinyota)Mwanza (mji)UyahudiWizara ya Mifugo na UvuviZuchuLilithSwalaWaheheAgostino wa HippoKishazi huruNgeliMuda sanifu wa duniaLiverpoolMaktabaSayansiWilaya ya ArushaPaul MakondaTambikoHistoriaKonsonantiUlimwenguMaji kujaa na kupwaMoscowKenyaKoroshoEl NinyoMimba za utotoniMuungano wa Tanganyika na ZanzibarKamusi za KiswahiliUzazi wa mpangoOrodha ya Magavana wa Tanganyika🡆 More