Afrika Ya Kiroma

Afrika hapo awali lilikuwa jina la jimbo la Dola la Roma katika mwambao wa Mediteranea huko Afrika Kaskazini miaka 146 KK - 698 BK.

Eneo lake lilikuwa takriban Tunisia ya kaskazini pamoja na pwani ya Libya ya magharibi na Algeria ya mashariki.

Afrika Ya Kiroma
Sarafu ya Kaisari Hadrian iliyotolewa kwa heshima ya jimbo la Africa. Mtu ambaye ni mfano wa Africa avaa kofia ya tembo.
Afrika Ya Kiroma
Dola la Roma mnamo 120 BK; jimbo la Afrika lina rangi nyekundu.
Afrika Ya Kiroma
Ramani ya jimbo mnamo 125 BK.

Jimbo lilikuwa maarufu kama "ghala ya ngano" ya Roma.

Watu wa Afrika ya Kaskazini kiasili walikuwa hasa Waberber.

Miji muhimu ilikuwa Karthago na Leptis Magna.

Bara la Afrika limepokea jina lake kutoka jimbo hili. Waarabu waliendelea kutawala eneo lake kwa jina la jimbo la Ifriqiya ambalo ni matamshi yao ya "Afrika".

Jina

Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale ambalo Waroma kwa jina hilo (Africa Proconsularis) hawakumaanisha bara lote bali eneo la Tunisia ya leo na kandokando yake upande wa Libya na Algeria.

Inasemekana asili ya jina hilo ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile, lakini kuna pia maelezo mengine tofautitofauti.

Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteraneo.

Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha labda nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

Tanbihi

Vyanzo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Afrika Ya Kiroma  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Afrika ya Kiroma kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Afrika Ya Kiroma JinaAfrika Ya Kiroma TanbihiAfrika Ya Kiroma Marejeo mengineAfrika Ya Kiroma Viungo vya njeAfrika Ya Kiroma146 KK698Afrika KaskaziniAlgeriaBKDola la RomaJimboJinaKaskaziniLibyaMagharibiMasharikiMediteraneaMwambaoPwaniTunisia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ManiiEkaristiSemantikiMadinaMkoa wa MwanzaMadiniVielezi vya namnaHekalu la YerusalemuYoweri Kaguta MuseveniUjimaAina za udongoMapambano kati ya Israeli na PalestinaOrodha ya MiakaTanganyikaPandaSkautiVitendawiliTabataMkondo wa umemeVidonda vya tumboHistoria ya KanisaRamaniKipaimaraWanyama wa nyumbaniTelevisheniKitabu cha ZaburiMpwaFananiIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)UbatizoMariooLigi Kuu Tanzania BaraMwanza (mji)IntanetiUgonjwa wa kupoozaDodoma (mji)Karne ya 18Vitenzi vishiriki vipungufuWikimaniaKaswendeNdoo (kundinyota)Injili ya MathayoKutoka (Biblia)MasharikiMuda sanifu wa duniaNomino za wingiSaharaIndonesiaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaChakulaDiniAgano JipyaMendeAlfabetiUlumbiVita vya KageraMalipoOrodha ya majimbo ya MarekaniJumuiya ya MadolaUshairiTenziMachweoMwanzoHistoria ya Kanisa KatolikiHafidh AmeirJokate MwegeloFalsafaHoma ya dengiWangoniTeknolojia ya habariSeli nyeupe za damuUtapiamloUkristoSaratani ya mlango wa kizaziUoto wa Asili (Tanzania)TashihisiDubai🡆 More