Wamisionari Wa Afrika

Wamisionari wa Afrika (kirefu Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika, kifupi zaidi M.

Afr.) ni jina rasmi la shirika la kimisionari la Kanisa Katoliki linalojulikana kwa Kiingereza kama "White Fathers" (kwa Kifaransa "Pères Blancs"), kutokana na rangi ya kanzu yao.

Wamisionari Wa Afrika
Kardinali Lavigerie, mwanzilishi wa shirika la kimisionari la White Fathers.

Lilianzisha mwaka 1868 na Charles Martial Lavigerie (1825-1892), askofu mkuu wa kwanza wa Algiers, Aljeria, ambaye baadaye akawa kardinali.

Lengo lilikuwa hasa uinjilishaji wa bara la Afrika, na kweli wanashirika walijitosa kufanya kazi kubwa ambayo inaendelea hata leo, ambapo lina mapadri kama 1,500.

Kisheria leo ni shirika la maisha ya kitume. Wanashirika hawaweki nadhiri kama watawa, ila kiapo cha kufanya umisionari kwa Waafrika hadi kifo chao.

Kwa agizo la mwanzilishi wao wanatakiwa kuishi katika jumuia yenye wamisionari kutoka nchi mbalimbali na kutumia hata kati yao lugha ya wenyeji.

Barua ya Lavigerie ya mwaka 1886 kwa Papa Leo XIII inasema: "Wao wanataka utawala, utaalamu na uchumi. Sisi basi, tujitahidi kuleta Ukristo na uhuru wa kweli. Afrika iwe nchi ya Waafrika, nao Waafrika wasigeuzwe kuwa Wazungu weusi." .

Tanbihi

Viungo vya nje

Wamisionari Wa Afrika  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamisionari wa Afrika kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Jina rasmiKanisa KatolikiKanzuKifaransaKifupiKiingerezaRangiShirikaUmisionari

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uandishi wa inshaLiverpoolMsamahaSwalaVirusi vya UKIMWIBabeliSamakiSayansiMitume wa YesuKukiMajigamboJinsiaKabilaMaishaOrodha ya mito nchini TanzaniaVielezi vya namnaBinadamuMsitu wa AmazonMnyoo-matumbo MkubwaUfahamuMange KimambiNdege (mnyama)Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)KukuMziziMajiWakingaMwanza (mji)BidiiMeno ya plastikiOrodha ya Marais wa UgandaHektariMtumbwiSteven KanumbaAina za manenoSayansi ya jamiiKishazi huruNevaNgeliVidonge vya majiraSanaa za maoneshoIndonesiaUpepoSemiMoyoWilaya ya NyamaganaMbooBendera ya KenyaUtawala wa Kijiji - TanzaniaMajira ya mvuaSomo la UchumiKiambishiAfrika ya Mashariki ya KijerumaniYesuNdoa katika UislamuWangoniUundaji wa manenoMkoa wa Dar es SalaamBongo FlavaUsawa (hisabati)Mkoa wa RuvumaAsidiWilaya ya IlalaWanyakyusaUhifadhi wa fasihi simuliziUkwapi na utaoMshororo🡆 More