Ugiriki: Nchi katika Ulaya Kusini-Mashariki

Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki cha kisasa: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Balkani.

Ugiriki

Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki. Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.

Jiografia

Kijiografia huwa na sehemu za Ugiriki bara, rasi ya Peloponesi upande wa kusini inayounganishwa kwa shingo ya nchi nyembamba, halafu visiwa vingi upande wa Bahari ya Aegean, Bahari ya Adria na kwenye Mediteranea yenyewe. Visiwa vikubwa zaidi ni Kreta, Euboea, Lesbo na Rhodos.

Historia

Ugiriki: Jiografia, Historia, Watu 
Parthenon, katika Akropoli ya Athens, ni kielelezo cha Ugiriki wa Kale.

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya" na kitovu cha Ustaarabu wa magharibi, kwa sababu ndipo vilipoanza demokrasia, falsafa ya magharibi, fasihi ya magharibi, historiografia, sayansi ya siasa, tafiti za sayansi na hisabati, tamthilia na michezo ya Olimpiki.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Watu

Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inayotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.

Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo (93%), hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (90%), halafu Waprotestanti na Wakatoliki. 2% ni Waislamu.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje


Nchi za Umoja wa Ulaya Ugiriki: Jiografia, Historia, Watu 
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Ugiriki: Jiografia, Historia, Watu  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ugiriki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ugiriki JiografiaUgiriki HistoriaUgiriki WatuUgiriki Tazama piaUgiriki MarejeoUgiriki Viungo vya njeUgirikiBalkaniKigirikiKusiniMasharikiRasiUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Koffi OlomideNamba tasaKiunzi cha mifupaMaishaChakulaMtakatifu PauloUtapiamloNamba za simu TanzaniaJoseph Leonard HauleMuundo wa inshaOrodha ya Marais wa UgandaMfumo wa upumuajiKisimaBikiraNimoniaKiarabuAir TanzaniaBaraKitenzi kikuuNgiriDr. Ellie V.DHassan bin OmariNapoleon Bonaparte27 MachiShirikisho la Afrika MasharikiShengMandhariHistoria ya WapareChelsea F.C.Idi AminTrilioniMotoZana za kilimoTungo kishaziKigoma-UjijiHistoria ya KanisaMalipoSilabiUgonjwaJihadiWiki FoundationIndonesiaKamusi ya Kiswahili sanifuMofimuMadiniSteven KanumbaUtandawaziKibodiNyangumiMaghaniDiniKanisa KatolikiWimboHaki za binadamuKumaAdhuhuriMajina ya Yesu katika Agano JipyaBata MzingaAbedi Amani KarumeVitenzi vishiriki vipungufuHaki za watotoJulius NyerereAzimio la ArushaFiston MayeleUkomboziDhahabuKatekisimu ya Kanisa KatolikiWabena (Tanzania)KunguniMapambano kati ya Israeli na PalestinaSomo la UchumiWashambaaKontuaNafsiMzabibuKylian MbappéViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)🡆 More