Ustaarabu wa magharibi ni utamaduni wenye taratibu za kijamii, maadili, desturi, sheria, falsafa, imani, siasa, sanaa na teknolojia maalumu ambavyo asili yake ni Ulaya hata kame vimezidi kustawi sehemu nyingine za dunia ambazo historia yake ilikuwa na uhusiano wa pekee na bara hilo.
Kwa kiasi kikubwa ni urithi wa Ugiriki wa Kale, Roma wa Kale, Uyahudi, na utamaduni wa makabila menginelakini hasa wa Ukristo na madhehebu yake ya kwanza, Kanisa Katoliki, pamoja na Makanisa ya Kiorthodoksi.
Baada ya Matengenezo ya Kiprotestanti, athari yake imekuwa kubwa pia, hasa Ulaya Kaskazini na makoloni yake, kama yale yaliyounda Marekani, ambayo katika karne ya 20 imeshika uongozi wa dunia na kuzidi kusambaza ustarabu huo.
Tabia yake ya msingi ni kujali na kustawisha akili badala ya kutegemea visasili na mapokeo. Ilikuwa hivyo kuanzia falsafa ya Shule ya Athene, ikaendelea baada ya uenezi wa Ukristo kupitia Teolojia ya Shule, Renaissance, Mapinduzi ya Kisayansi hadi Falsafa ya Mwangaza. Hiyo ilisaidia kutambua tunu kama haki za binadamu, usawa na demokrasia.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ustaarabu wa magharibi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ustaarabu wa magharibi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.