Jihadi

Jihadi ni neno lenye asili ya Kiarabu (‏جهاد‎ jihād) na lenye maana ya kujitahidi kwa ajili ya Allah katika dini ya Uislamu.

Jihadi
Kikundi cha waasi wa Kiislamu nchini Mali

Mtu anayehusika katika jihadi huitwa "mujahid". Jihadi ni wajibu wa kidini kwa Waislamu.

Jihadi katika Qurani

Katika Qurani neno jihadi linapatikana mara 41, mara nyingi katika usemi "jihadi kwenye njia ya Mungu (الجهاد في سبيل الله al-jihad fi sabil Allah)".. Katika Qurani "jihadi" huwa hasa na maana ya kijeshi lakini si wazi kama maana hiyo ilikuwa mapigano dhidi ya wenye imani tofauti kwa jumla au vita vya kujihami tu.

Jihadi katika mafundisho ya wataalamu wa shari'a

Katika mafundisho ya wataalamu Waislamu wa karne za kwanza baada ya Muhammad jihadi ilikuwa na shabaha ya kupanua eneo chini ya utawala wa Uislamu na utetezi wake, hadi Uislamu ugeuke dini rasmi.

Hii haikuwa na shabaha ya kuwalazimisha wote wasiokuwa Waislamu kupokea dini hiyo. Katika mafundisho ya wataalamu wa kale, wale walioitwa "Wapagani" walipaswa kushambuliwa hadi wakubali Uislamu au wauawe. Lakini watu wa "ahl al-kitab" (wenye misahafu) yaani Wakristo, Wayahudi na Wasabayi walipewa nafasi ya kukubali kipaumbele cha Waislamu na kuishi chini ya utawala wa Waislamu katika hali ya dhimma.

Katika mwendo wa upanuzi wa utawala wa Kiislamu nafasi ya dhimma iliongezwa pia kwa dini nyingine kama Uzoroastro na Uhindu ingawa hao wana miungu mingi sana.

Mwishoni karibu kila jumuiya ya kidini ilipewa nafasi ya kukubali hali ya dhimma.

Jihadi kati ya Waislamu wa leo

Leo hii jihadi ina maana tatu kati ya Waislamu, hasa

  1. kutetea imani ya Kiislamu pamoja na kulinda umma ya Waislamu, pia kutetea Waislamu wanaoshambuliwa
  2. kushindana na udhaifu wa nafsi na kujitahidi kuwa mtu mwema
  3. jitihada za kuboresha umma ya Waislamu.

Waislamu kadhaa wanaitumia pia kwa maana ya kueneza Uislamu kwa njia ya silaha na matishio. Hapo kuna hata makundi kama Al Qaida na Boko Haram wanaotumia mbinu za ugaidi kwa jihadi jinsi wanavyoielewa. Ingawa idadi yao si kubwa kati ya Waislamu kwa jumla, watu wengi nje ya Uislamu wanaelewa neno hasa kwa maana inayotangazwa na hao.

Tanbihi

Kujisomea

Jihadi  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Jihadi katika QuraniJihadi katika mafundisho ya wataalamu wa shariaJihadi kati ya Waislamu wa leoJihadi TanbihiJihadiAllahAsiliDiniKiarabuNenoUislamu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kanye WestMaajabu ya duniaRita wa CasciaSiasaMfumo wa JuaNgiriUsanifu wa ndaniMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaKabilaNgamiaHadithi za Mtume MuhammadMajina ya Yesu katika Agano JipyaHekalu la YerusalemuOrodha ya Marais wa KenyaOrodha ya kampuni za TanzaniaPijiniSodomaKanisaMbeyaSimbaMkoa wa MbeyaMkoa wa KageraChama cha MapinduziWashambaaSayansi ya jamiiTanganyika (maana)ShairiUkristo nchini TanzaniaUongoziPemba (kisiwa)Wema SepetuUNICEFNahauKiarabuUtumbo mwembambaWanyama wa nyumbaniUtandawaziMkutano wa Berlin wa 1885SentensiPunyetoMartin LutherMpira wa miguuMvua ya maweJuxVichekeshoMzeituniHali ya hewaSabatoBarua pepeAli Hassan MwinyiBinadamuKinyongaRejistaWilaya za TanzaniaUjerumaniUharibifu wa mazingiraInsha za hojaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoWahadzabeKifaruUtumbo mpanaKataIsimujamiiFigoUlimwenguUkoloniMfuko wa Mawasiliano kwa WoteMillard AyoDiglosiaTanzaniaAsidiDubai (mji)Kiwakilishi nafsiAfrika KusiniMbuni🡆 More