Vita Ya Miaka Saba

Vita ya Miaka Saba ilitokea kati ya miaka 1756 na 1763.

Ilitokana na mashindano ya nchi za Ulaya ikasambaa pande nyingi za dunia. Hivyo imeitwa "Vita Kuu ya Dunia" ya kwanza hata kama jina hilo kwa kawaida linatumiwa kwa ajili ya vita kati ya 1914 na 1918.

Vita Ya Miaka Saba
Maeneo yote yaliyoathiriwa na Vita ya Miaka Saba      Uingereza, Prussia, Ureno na nchi ndogo      Ufaransa, Hispania, Austria, Urusi, Uswidi, pamoja na koloni na nchi ndogo upande wao
Vita Ya Miaka Saba
Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya mwanzoni wa vita ya miaka 7.

Washiriki

Washiriki katika vita hii walikuwa nchi za Ulaya na makoloni yao, pia watu wa sehemu mbalimbali za dunia walioshikamana nao.

Walipopigana walikuwa:

Sababu za vita

Vita ilianza kwa sababu mbili hasa:

  • ndani ya Amerika ya Kaskazini Ufaransa na Uingereza zilishindana kuhusu upanuzi wa maeneo yao.
  • katika Ulaya Prussia iliwahi kutwaa jimbo la Silesia kutoka Austria na Austria ilitaka kuchukua jimbo hilo tena.
  • nchi nyingi za Ulaya ziliogopa uwezo mkubwa mno wa nchi nyingine ikiruhusiwa kushinda vitani, hivyo ziliamua kuingilia kati.

Mashindano na hofu hizo vilisababisha kutokea kwa makambi hayo mawili makubwa.

Vita Ya Miaka Saba 
Vituo vikuu vya Waingereza (nyekundu) na Wafaransa (buluu) katika Uhindi kabla ya vita

Mapigano

Mapigano yalitokea Ulaya hasa Ujerumani, halafu huko Uhindi, Amerika ya Kaskazini, kwenye visiwa vya Karibi, pwani za Afrika na Ufilipino.

  • Uingereza ilitwaa "Ufaransa Mpya" (sehemu ya Kifaransa ya Kanada ya leo) na kuwafukuwa Wafaransa kutoka maeneo ya magharibi ya koloni lao hilo.
  • Katika Karibi Waingereza walitwaa visiwa vingi vya Wafaransa isipokuwa Martinique na Guadeloupe.
  • Katika Uhindi vituo vingi vya Ufaransa vilitwaliwa isipokuwa Pondicherry iliyobaki kama koloni dogo la Ufaransa (hadi 1960). Waingereza kwa kutwaa kipaumbele katika Ubengali waliweka msingi wa utawala wao wa baadaye juu ya Uhindi wote.
  • Katika Afrika Waingereza walitwaa kituo cha St. Louis katika Senegal kutoka Ufaransa (ilirudishwa baada ya vita)
  • Prussia iliweza kutetea jimbo la Silesia dhidi ya Austria ikapata sifa nyingi kwa sababu jeshi lake lilishindana na Waaustria, Warusi na Wafaransa kwa wakati mmoja. Lakini mnamo mwaka 1762 nguvu za Prussia zilikwisha ikaelekea kushindwa. Iliokolewa kwa sababu malkia Elizabeti wa Urusi alifariki na mfalme mpya Petro III alimpenda sana mfalme wa Prussia akaamua kupatana naye badala ya kumshambulia tena. Hivyo Austria ilibaki adui pekee ikashindwa.
Vita Ya Miaka Saba 
Vita ya miaka 7 katika Amerika ya Kaskazini
buluu: eneo la Kifaransa; nyekundu: eneo la Kiingereza kabla ya vita; Ufaransa ilipoteza yote

Matokeo

Matokeo makuu ya vita

  • Uingereza ilipata kuwa nchi yenye makoloni mengi zaidi duniani baada ya Hispania ikaelekea kuipiku. Pia ilitawala bahari za dunia kwa kuwa taifa lenye manowari mengi na vituo pamoja na bandari kwenye mabara yote.
  • Uwezo wa Ufaransa ulipunguzwa ikipotewa na makoloni yake katika Amerika ya Kaskazini na kubaki na maeneo madogo tu katika Karibi na Uhindi.
  • Prussia ilitoka vitani kama nchi muhimu ya tano ya Ulaya pamoja na Ufaransa, Austria, Uingereza, na Urusi.

Matokeo ya baadaye

  • Msingi wa Kiingereza kuwa lugha ya kwanza duniani uliwekwa kwa sababu kilitumiwa kote katika makoloni ya Uingereza
  • Ushindi wa Uingereza ulikuwa msingi wa mapinduzi na uhuru wa Marekani miaka 13 baadaye. Walowezi walijifunza mitindo ya vita waliposhiriki katika vita upande wa Uingereza na walitumia ujuzi huo baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipunguza vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya Kaskazini.
  • Uadui wa Ufaransa dhidi ya Uingereza ulibaki ukaimarishwa na kusababisha usaidizi wa Ufaransa kwa waasi wa Amerika ya Kaskazini mwaka 1776 hadi kuzaliwa kwa taifa jipya la Marekani.
  • Kudhoofishwa kwa Ufaransa kwa sababu ya gharama kubwa ya vita hivyo na ile ya kusaidia Wamarekani baadaye ambayo iliathiri uchumi na sifa za utawala wa kifalme na kuwa sababu muhimu ya mapinduzi ya Kifaransa
  • Ushindi wa Prussia ulisababisha mashindano ya mfululizo kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele katika Ujerumani yaliyoonekana baadaye hadi vita ya 1866.

Picha za watawala wa nchi shiriki za Vita ya miaka saba

Tazama pia

Vita Ya Miaka Saba  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Miaka Saba kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Vita Ya Miaka Saba WashirikiVita Ya Miaka Saba Sababu za vitaVita Ya Miaka Saba MapiganoVita Ya Miaka Saba MatokeoVita Ya Miaka Saba Picha za watawala wa nchi shiriki za Vita ya miaka sabaVita Ya Miaka Saba Tazama piaVita Ya Miaka Saba17561763DuniaJinaUlayaVita Kuu ya DuniaVita Kuu ya Kwanza ya Dunia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MariooViwakilishi vya urejeshiMnyoo-matumbo MkubwaBikira MariaUtumbo mpanaTreniMuhammadMahakamaTovutiRaiaDar es SalaamMwanaumeMilaUpinde wa mvuaIniNambaVita vya KageraMaishaRitifaaWaziriImaniNgiriWilaya ya KinondoniUtamaduniAnwaniSomo la UchumiMbezi (Ubungo)Ngw'anamalundiMjombaMaktabaWahaCleopa David MsuyaMbooJumuiya ya Afrika MasharikiMaana ya maishaKukiAgano JipyaHarmonizeKaswendeVieleziStashahadaMartha MwaipajaHalmashauriShukuru KawambwaMaadiliKamusiUchumiOrodha ya viongoziPasifikiLiverpool F.C.Magonjwa ya machoMfumo katika sokaSkeliKondomu ya kikeSteven KanumbaTiktokWanyakyusaNomino za jumlaKata za Mkoa wa MorogoroChuo Kikuu cha Dar es SalaamAmfibiaKutoa taka za mwiliSitiariSanaaFonolojiaMaajabu ya duniaUvimbe wa sikioMashuke (kundinyota)LafudhiTanganyika (ziwa)Ligi Kuu Uingereza (EPL)Tungo kishaziUshairi🡆 More