Visiwa Vya Falkland

Visiwa vya Falkland (kwa Kiingereza: Falkland Islands; kwa Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban km 450 mbele ya pwani ya Argentina.

Visiwa vya Falkland
Visiwa Vya Falkland
Kanisa kuu la Christchurch, Stanley.
Visiwa Vya Falkland
Nyumba ya mkulima katika nyika za Falkland.

Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.

Jiografia

Funguvisiwa lina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban km² 6,000. Mwinuko mkubwa ni mlima Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) wenye kimo cha mita 708 juu ya uwiano wa bahari.

Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hiyo mimea ni hasa nyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.

Watu

Idadi ya wakazi imepita 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki zao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo.

Upande wa dini, 66% ni Wakristo, hasa Waanglikana, lakini pia Wakatoliki na wengineo. 32% hawana dini yoyote.

Mji pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki wenye wakazi 2,100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500.

Barabara ya lami ya pekee kisiwani ni ile inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje

Visiwa Vya Falkland 
WikiMedia Commons
Visiwa Vya Falkland  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Falkland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Visiwa Vya Falkland JiografiaVisiwa Vya Falkland WatuVisiwa Vya Falkland TanbihiVisiwa Vya Falkland MarejeoVisiwa Vya Falkland Viungo vya NjeVisiwa Vya FalklandArgentinaAtlantikiBahariFunguvisiwaKihispaniaKiingerezaKmKusiniPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MahakamaUzazi wa mpangoManeno sabaMafarisayoMuundo wa inshaFani (fasihi)Njia ya MsalabaNyokaRwandaUtapiamloAbrahamuMungu ibariki AfrikaUkoloniNgonjeraSumakuRamadan (mwezi)Kishazi tegemeziHistoria ya EthiopiaTafsiriBaruaMkoa wa MtwaraMaji kujaa na kupwaSteve MweusiVirusiMpwaAfrika ya MasharikiNelson MandelaSarufiMauaji ya kimbari ya RwandaUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiMwanzoAzimio la ArushaItikadiNyaniUhifadhi wa fasihi simuliziNyati wa AfrikaCristiano RonaldoTungo kiraiMadawa ya kulevyaShetaniTwigaTashdidiMbwana SamattaRushwaLeopold II wa UbelgijiWaluguruUchimbaji wa madini nchini TanzaniaNileSaida KaroliKitubioSayansiBunge la Afrika MasharikiBungeChuraWilaya za TanzaniaTabainiOrodha ya vitabu vya BibliaKamusiPonografiaKiumbehaiMashariki ya KatiRaiaMkanda wa jeshiUkooWayback MachineAshokaMazungumzoKrismasiWhatsAppKiungo (michezo)UkomboziKaabaMbeya (mji)ArudhiFonolojia🡆 More