Twitter

Twitter ilikuwa mtandao wa kijamii wa kutoa huduma ya kutuma vijiujumbe vidogo vinavyoitwa Tweets na kushea na watu wanaokufuata.

Unamilikiwa na kampuni ya Marekani Twitter, Inc. Watumiaji wanatumia simu za mkononi au kompyuta kutuma na kusoma jumbe. Tweet zinaweza kuwa na maneno yenye urefu wa 140 tu. Hata hivyo mwaka 2017 kampuni hii ilitangaza kuongeza idadi ya urefu wa maneno hadi 280. Maneno haya au jumbe hizi zinaonekana katika ukurasa wa mtumiaji. Tweet hizi aghalabu zinaweza kusomwa na mtu yeyote, lakini mtumaji anaweza pia kuzifanya ziwe faragha. Tweet ambazo ni faragha zinaweza kuonekana kwa wale ambao wanakufuata tu.

Twitter
Logo ya Twitter kabla ya kubadilishwa kuwa X.

Watumiaji wanaweza kujiandikisha na kutweet kwa watu wengine. Mtindo huo unaitwa following au kufuata, na wanaojiandikisha wanaitwa followers au wafuasi. Mwishoni mwa mwaka wa 2009, watumiaji waliweza kufuata orodha za muumbaji.

Watumiaji wanaweza kupokea tweets kwa kutumia wavuti ya Twitter. Vilevile wanaweza kutumia programu pepe ambazo zinafanya kazi na Twitter kwenye simujanja.

Twitter ilianzishwa na Jack Dorsey, Noah Glass, Biz Stone, na Evan Williams mnamo Machi 2006 na kuzinduliwa mnamo Julai mwaka huo huo. Twitter, Inc. ina makao yake makuu San Francisco, California na ina zaidi ya ofisi 25 duniani kote. Kufikia mwaka wa 2012, twitter ilikuwa na watumiaji zaidi ya milioni 100 na walituma tweets milioni 340 kwa siku. Mnamo mwaka wa 2013, ilikuwa mojawapo ya tovuti kumi zilizotembelewa zaidi. Kufikia mwanzoni mwa 2019, Twitter ilikuwa na zaidi ya watumiaji milioni 330.

Historia

Twitter ilianzishwa tarehe 21 Machi mwaka 2006, na Jack Dorsey, Biz Stone, na Evan Williams huko San Francisco, California, Marekani. Jukwaa hilo lilizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka huo huo. Twitter ilipata umaarufu haraka kutokana na muundo wake wa ujumbe mfupi, maarufu kama "tweets," ambayo awali ilikuwa na kikomo cha herufi 140. Kikomo hicho kiliondolewa mnamo Novemba 2017, likiruhusu watumiaji kutuma ujumbe wa herufi 280.

Twitter ilikuwa jukwaa la kwanza kuanzisha mfumo wa kufuatilia (follow) na kuwa na mtiririko wa wakati halisi wa matukio (timeline). Watumiaji wanaweza kutoa maoni kwa kutumia alama ya "@" kwa kumtaja mtumiaji mwingine, na pia kutumia alama ya "hashtag" (#) ili kuchangia katika mazungumzo yanayohusiana na mada fulani.

Tangu kuanzishwa kwake, Twitter imekuwa chombo muhimu cha mawasiliano, kutoa jukwaa la kutoa maoni, kushiriki habari, na kusambaza mazungumzo ya ulimwengu. Imetumika kwa kampeni za kisiasa, mawasiliano ya dharura, na kuleta pamoja watu kutoka maeneo mbalimbali duniani. Pia, imeshuhudia mabadiliko kadhaa kwenye jukwaa hilo, pamoja na marekebisho ya sera na kuboresha kwa vipengele vyake.

Tanbihi

Viungo vya nje

Tags:

KompyutaMtandao wa kijamiiSimu za mkononi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ChakulaTanganyika (ziwa)Ng'ombeAina za manenoSarufiUzazi wa mpangoMafua ya kawaidaWayahudiLigi ya Mabingwa UlayaNdovuBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiWahaAnwaniUsafi wa mazingiraTabianchi ya TanzaniaTanganyika African National UnionWabena (Tanzania)Mfumo wa mzunguko wa damuKanisaMkoa wa IringaAbrahamuRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMimba kuharibikaTwigaChamaziAntibiotikiNahauVita ya Maji MajiBagamoyo (mji)Uenezi wa KiswahiliMwanzoPombooMtakatifu MarkoMnyamaMrijaSerikaliKukuTetemeko la ardhiClatous ChamaMpira wa kikapuKiwakilishi nafsiUfisadiMwenge wa UhuruMkoa wa ManyaraKitenzi kikuu kisaidiziTenzi tatu za kaleUtandawaziEdward SokoineUtamaduni wa KitanzaniaHistoria ya WapareSimbaMisriAfrika ya MasharikiIntanetiUkimwiOrodha ya visiwa vya TanzaniaNangaMofimuMoses KulolaKibu DenisBendera ya TanzaniaSaida KaroliBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiSaidi Salim BakhresaBunge la TanzaniaNduniUandishi wa inshaElimu ya bahariInsha za hoja🡆 More