Leopold Sedar Senghor

Léopold Sédar Senghor (9 Oktoba 1906 – 20 Desemba 2001) alikuwa mshairi, mwanasiasa na hatimaye rais wa kwanza wa Senegal kati ya miaka 1960 na 1980.

Léopold Sédar Senghor
Leopold Sedar Senghor

Rais wa kwanza wa Senegal
Muda wa Utawala
6 Septemba 1960 – 31 Disemba 1980
Waziri Mkuu Abdou Diouf
mtangulizi Office created
aliyemfuata Abdou Diouf

tarehe ya kuzaliwa (1906-10-09)9 Oktoba 1906
Joal, Afrika ya Magharibi ya Kifaransa (leo Senegal)
tarehe ya kufa 20 Desemba 2001 (umri 95)
Verson, Ufaransa
chama Chama cha Kisoshalisti cha Senegal
ndoa Ginette Éboué (1946-1956)
Colette Hubert Senghor (m. 1957–2001) «start: (1957)–end+1: (2002)»"Marriage: Colette Hubert Senghor to Leopold Sedar Senghor" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Leopold_Sedar_Senghor);hadi kifo
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Paris
dini Kanisa Katoliki
signature Leopold Sedar Senghor

Senghor alikuwa Mwafrika wa kwanza aliyechaguliwa kuwa mwanachama wa Académie française. Kabla ya uhuru wa nchi yake aliunda chama cha Umoja wa Kidemokrasia wa Senegal (kwa Kifaransa: Bloc démocratique sénégalais; kwa Kiingereza: Senegalese Democratic Bloc). Wengi wanamhesabu kati ya wataalamu Waafrika muhimu zaidi katika karne ya 20.

Maisha

Senghor alizaliwa katika kijiji cha Joal kilichowahi kuwa kati ya vituo vya kwanza vya wafanyabiashara kutoka Ulaya na pia kitovu cha misheni Za Kanisa Katoliki kwenye pwani ya Senegal. Baba yake alikuwa mfanyabiashara mzalendo, mama yake mke wa tatu wa baba na Muislamu.

Alipokuwa na umri wa miaka 8 alianza kusoma shule ya mapadre akaendelea kwenye seminari ya mapadri wa Roho Mtakatifu na baada ya kushauriwa asiendelee na masomo ya upadre alisoma shule ya kawaida.

Alimaliza vema hasa kwa masomo ya Kifaransa na Kilatini akapewa nafasi ya kusoma chuo Ufaransa .

Mwaka 1928 Senghor alikwenda Ufaransa aliposoma lugha na baadaye sarufi ya Kifaransa kwenye Chuo Kikuu cha Paris. Baada ya masomo alipewa nafasi ya kufundisha kwenye vyuo vya Tours na Paris. Mwaka 1932 alipata uraia wa Ufaransa.

Tangu siku zake masomoni alikuwa na urafiki na Aime Cesaire na pamoja naye alibuni hoja ya "negritude" walipotetea kuwepo kwa utamaduni wa "Watu Weusi" kama utamaduni wa pekee na muhimu, tofauti na utamaduni wa Kizungu.

Mwaka 1945, baada ya vita vikuu vya pili na ushindi wa Ufaransa, alijiunga na chama cha kisoshalisti akachaguliwa kuwa mbunge.

Mwaka 1960 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Senegal akaendela kushika nafasi hiyo hadi mwaka 1980 alipong'atuka kwa hiari.

Marejeo

Leopold Sedar Senghor  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leopold Sedar Senghor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Bd

Tags:

19061960198020 Desemba20019 OktobaMshairiMwanasiasaRaisSenegal

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Injili ya MathayoTovutiDubaiHadithi za Mtume MuhammadHarusiChuiWhatsAppIdi AminDakuOsimosisiCAFKunguniUtenzi wa inkishafiKalenda ya KiislamuMapinduzi ya ZanzibarMtende (mti)ShambaUgonjwa wa kupoozaMarekaniMillard AyoWayao (Tanzania)RamaniKitabu cha ZaburiMacky SallMuhammadUandishiJackie ChanAzimio la kaziVitendawiliJulius NyerereARupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMjasiriamaliIntanetiInstagramMunguFasihiMizimuOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKichochoUtegemezi wa dawa za kulevyaMlongeLigi ya Mabingwa AfrikaKigoma-UjijiShereheRushwaMekatilili Wa MenzaUingerezaWapareWizara za Serikali ya TanzaniaImaniLuis MiquissoneWabena (Tanzania)UgaidiMofolojiaNdoaAthari za muda mrefu za pombeSaratani ya mapafuAina za udongoOrodha ya vyama vya kisiasa nchini KenyaMkoa wa DodomaIsraeli ya KaleMwenge wa UhuruMnururishoDamuMkoa wa MwanzaUkwapi na utaoUlumbiNguvaArsenal FCJakaya KikweteMalipoKairo🡆 More