Kitongoji Duni

Kitongoji duni (pia: mtaa wa vibanda; kwa Kiingereza slum) ni mtaa jijini ambao mara nyingi huwa na nyumba duni zilizosimikwa karibu, miundomsingi duni na wakazi maskini.

Huduma za usambazaji wa maji safi, umeme na usalama huwa adimu. Vitongoji duni mara nyingi hupatikana mijini katika nchi zinazokua kimaendeleo kwa sababu ya kiwango kikuu cha ukuaji na uhamiaji.

Sifa za vitongoji duni

Mahali na Ukuaji

Kitongoji Duni 
Vyoo vya kulipia katika vitongoji duni vya Mukuru, Nairobi.

Vitongoji duni huanzia pambizoni mwa miji karibu au katika ardhi ambazo hazina thamani kubwa, ni za serikali au milki ya ufadhili au taasisi ya dini au hazina hatimiliki hakika. Baadhi ya vitongoji duni hujipa majina ya vyama vya kisiasa, watu tajika kihistoria, wanasiasa ama watu waliokuwa wamiliki wa ardhi hiyo. Kwa mfano, vitongoji duni Mukuru kwa Njenga na Mukuru kwa Ruben.

Kutokuwa na uhakika wa umiliki wa ardhi

Baadhi ya wahamiaji huchukulia ardhi ambayo haina wakazi kuwa haina wamiliki na hivyo basi wakapakaa.Serikali pia inaweza kugawia watu ploti na baadaye ardhi hiyo ikabadilika kuwa kitongoji duni na watu kupoteza haki ya kudai ploti. Kwa mfano, Kibera.

Makazi duni

Vitongoji duni huwa na vyumba duni. Mara nyingi, ubora wa vyumba hauwezi kustahimili mvua nyingi au upepo mkali. Vifaa vya ujenzi huwa karatasi, plastiki n.k. Sakafu za mchanga, kuta za matope, mbao zilizoshikiliwa kwa kamba, au mabati. Hata wakati nyumba zimejengwa kwa mawe na simiti, hakuna umakinifu katika muundo na uhandisi wa jengo na hivyo basi, majengo hayo hayazingatii kanuni za serikali za ujenzi. Nyumba hizo pia huwa zimejengwa karibu sana.

Miundomsingi isiyotosha

Vitongoji duni huwa havina miundomsingi ya kutosha. Kama vile, maji safi, umeme, huduma za afya, usalama na polisi, usafiri wa umma, huduma za zimamoto, ambulensi, mfumo wa majitaka na barabara sakifu.

Uenezi

Kitongoji Duni 
Asilimia ya wakazi wa vitongoji duni katika miji ya kila nchi. (Asili: UM HABITAT 2005).

Vitongoji duni ni tatizo la dunia nzima.

Picha

Tanbihi

Kitongoji Duni  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitongoji duni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kitongoji Duni Sifa za vitongoji duniKitongoji Duni UeneziKitongoji Duni PichaKitongoji Duni TanbihiKitongoji DuniJijiKiingerezaMaskiniMtaaNyumbaen:slum

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Biashara ya watumwaKitenziDhahabuWasafwaKiraiBaruaNomino za pekeeUsultani wa ZanzibarMombasaLughaOrodha ya Marais wa TanzaniaMkoa wa TangaKutoka (Biblia)Mkoa wa MorogoroKunguruWiki CommonsMaghaniJulius NyerereMongoliaWairaqwZama za MaweUbaleheKunguniVielezi vya mahaliUzazi wa mpango kwa njia asiliaWamasaiNetiboliOrodha ya MiakaLugha za KibantuWachaggaKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaHekaya za AbunuwasiJiniMaajabu ya duniaNamba za simu TanzaniaJackie ChanKisasiliMkoa wa ArushaHaki za binadamuZana za kilimoLilithYuda IskariotiAunt EzekielOrodha ya makabila ya TanzaniaVirusiUrusiNgonjeraBiblia ya KikristoNyanda za Juu za Kusini TanzaniaKombe la Dunia la FIFATetekuwangaFiston MayeleUtafitiElimuMofimuNguzo tano za UislamuNairobiVieleziKuraniJumapili ya matawiAfrika ya Mashariki ya KijerumaniKitenzi kikuuMkoa wa Dar es SalaamHekalu la YerusalemuKadi za mialikoSikioJogooManchester CityAsiliFonetikiUtapiamloSeli nyeupe za damuUkabailaJumuiya ya Afrika MasharikiAndalio la somoMwenyekiti🡆 More