Kichapishi

Kichapishi (kutoka kitenzi kuchapa; pia: printa, kutoka Kiingereza printer) ni kifaa kimojawapo cha kompyuta.

Inaruhusu mtumiaji kuchapisha maandishi kwenye karatasi, kama vile barua na picha.

Kichapishi cha IBM
Kichapishi cha IBM

Kwa kawaida kichapishi kipo chini ya udhibiti wa kompyuta yaani, inaendeshwa na kompyuta.

Wengi wanaweza pia kuifanya kazi kama mashine ya kutoa nakala kwa kutumia kichapishi au kwa kutumia kamera ya kidijiti ili kuchapisha moja kwa moja bila kutumia kompyuta.

Aina

  1. Vichapishi vya mgongano (impact printers) hutumia vifaa mbalimbali vinavyopiga riboni inayopeleka wino kwenye karatasi. Vimepitishwa na vichapishi vya kisasa zaidi havitumiwi sana tena. Isipokuwa vichapishi vya sindano (dot-matrix printers) bado hutumiwa katika ofisi kwa sababu zinaweza kutoka nakala ya pili mara moja au kujaza fomu zilizochapishwa tayari. Kichapishi cha sindano huchora nukta nyingi zinazounda umbo la herufi.
  2. Kichapishi cha wino (inkjet printer) huwa na nozeli inayosogezwa haraka juu ya karatasi na kupuliza matone madogo ya wino kwene uso wake. Kwa njia hiyo inachora haraka herufi na pia picha. Mashine hizo ziapatikana kwa matumizi na rangi moja -kwa kawaida nyeusi- au rangi nne zinazounganishwa kuunda rangi nyingi. Vichapishi vya wino hupatikana kwa bei nafuu lakini mara nyingi wino yake huuzwa ghali. Sokoni kuna wino mbadala kwa bei nafuu lakini kuna uwezekano kwamba wino fulani haulingani na kifaa chenyewe.
  3. Kichapishi cha leza (laser printer) hutumia silinda yenye chaji ya umeme na wino ya unga. Mwanga wa leza hupita juu ya silinda na kubadilisha chaji kwenye uso wake hivyo kuchora picha ya matini au uchoraji. Wino yenye umbo la unga hupulizwa kwenye silinda na kushika kwenye sehemu zilizoathiriwa na leza. Karatasi hupitishwa kwenye silinda na kupokea wino ya unga. Karatasi inapita kwenye silinda ya joto ambako wino huwa imara. Mtindo huu kimsingi ni sawa na mfumo wa fotokopi.
  4. Kichapishi cha 3D kinatengeneza nakala ya vitu vyenye pandeolwa tatu. Mara nyingi hutumia plastiki na kujenga matokeo yake tabaka baada ya tabaka. Vichapishi vya 3D vya kiwandani hutumia pia metali au mata nyingine. Mashine kubwa huchapisha vitu vikubwa hadi nyumba.
  5. Printamtandao huweza kufikiwa na yeyote kupitia mtandao
  6. Printashiriki hupokea maagizo ya tarakilishi zaidi ya moja, ingawa kwa wakati mmoja huchapa kazi ya mojawapo tu.

Tanbihi

Kichapishi  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BaruaKaratasiKifaaKiingerezaKitenziKompyutaMaandishiPicha

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TashihisiAdolf HitlerWakingaTulia AcksonBendera ya KenyaUrusiVivumishi vya sifaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaMwamba (jiolojia)Ugonjwa wa kuharaUchumiPumuIsimujamiiSikioKitenzi kishirikishiUkwapi na utaoDawa za mfadhaikoHistoria ya KiswahiliBahashaJamhuri ya Watu wa ZanzibarTungo kishaziUjerumaniSikukuu za KenyaAsili ya KiswahiliShairiMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaKarafuuUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaVitenzi vishiriki vipungufuNgeliJamhuri ya Watu wa ChinaWaziriUvimbe wa sikioOrodha ya nchi za AfrikaSamakiKamusi za KiswahiliMsokoto wa watoto wachangaSteven KanumbaWanyamaporiVielezi vya namnaHarmonizeMnururishoKitenzi kikuu kisaidiziLionel MessiMkoa wa SimiyuOrodha ya mito nchini TanzaniaWaluguruSentensiMapenzi ya jinsia mojaUislamuSaidi NtibazonkizaKhalifaKifua kikuuHistoria ya WapareSerikaliSaida KaroliJuxUenezi wa KiswahiliSarufiAndalio la somoDhima ya fasihi katika maishaMisimu (lugha)Uzazi wa mpangoStashahadaUkristo nchini TanzaniaKata za Mkoa wa MorogoroJinsiaMkoa wa PwaniC++Mkoa wa MorogoroMbeya (mji)UlimwenguMadiniUfugaji wa kukuIfakara🡆 More