Homa Ya Q

Homa ya Q ni ugonjwa unaosababishwa na Coxiella burnetii, bakteria anayeathiri binadamu na wanyama.

Q fever
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A78.
ICD-9083.0
eMedicinemed/1982 ped/1973
MeSHD011778

Bakteria hiyo si ya kawaida ila inaweza kupatikana katika ng'ombe, kondoo, mbuzi na mamalia wengine wafugwao, ikiwa ni pamoja na paka na mbwa. Maambukizi hutokana na kuvuta pumzi yenye chembechembe zilizosindikwa katika hewa, na kugusa maziwa, mkojo, kinyesi, majimaji ya uke, au shahawa za wanyama walioambukizwa. Mara chache, ugonjwa huo hutokana na kupe.

Muda mpaka ugonjwa utokee ni siku 9-40. Unaweza kuchukuliwa kama ugonjwa ambao ni rahisi kupata maambukizi duniani, kwa sababu mwanadamu anaweza kuambukizwa na bakteria moja. Bakteria hiyo huishi katika mazingira maalumu ndani ya mwili.

Historia

Homa Ya Q 
Image A:X-ray ya kawaida ya kifua. Image B: Homa ya Q ya mapafu.

Mara ya kwanza ulielezwa na Edward Holbrook Derrick katika machinjio ya Brisbane, Queensland, Australia. Herufi "Q" husimama kwa "query" na ilitumika wakati kimelea kisababishi hakijulikani, na iliteuliwa baada ya mapendekezo kama, "homa ya machinjio" na "homa ya Queensland rickettsial", ili kuepuka ukinzani mbaya, aidha katika sekta ya mifugo au jimbo la Queensland.

Bakteria ya homa ya Q iligundulika mwaka 1937, wakati Frank Burnet MacFarlane na Mavis Freeman walipoitenganisha kutoka kwa mmoja wa wagonjwa wa Derrick. Awali ilitambuliwa kama aina ya Rickettsia.

HR Cox na Davis waliitenganisha kutoka kwenye kupe kule Montana, Marekani mwaka 1938. Ni ugonjwa wa wanyama,ambao unapatikana sanasana kwenye ng'ombe, kondoo na mbuzi. Coxiella burnetii hachukuliwi kama anahusiana kwa karibu na Rickettsiae bali ni kama sawa na Legionella na Francisella na ni bakteria ya kwenye protini.

Muonekano

Muda mpaka utokee ni wiki kati ya 2 mpaka 3. Kwa kawaida hutokea kama dalili ya mafua ikiambatana na utokeaji wa haraka wa homa, mwili kutokuwa katika hali ya kawaida, jasho, kuumwa kichwa sana, myalgia (maumivu ya misuli), maumivu ya maungio, kupoteza hamu ya chakula, matatizo ya kupumua, kukohoa kikohozi kikavu, maumivu ya kuvimba kwa plura, baridi, kuchanganyikiwa na dalili zitokanazo na njia ya chakula kama vile kichefuchefu, kutapika na kuhara. Homa huchukua takriban siku 7-14.

Kadiri ugonjwa unavyokuwa nao, unaweza kuendelea na kuwa nimonia isiyo na dalili kamili, na kuweza kuleta tatizo litishialo uhai la upumuaji dhiki (ARDS), ambapo dalili hutokea katika siku 4 mpaka 5 za maambukizi.

Nadra sana, homa ya Q husababisha (granulomatous) homa ya manjano ambayo yaweza kuwa haina dalili au kuwa na dalili kama malaise, homa, ini kuvimba (hepatomegaly) na maumivu katika quadrant juu, kulia, ya tumbo. Wakati matatizo ya transaminase mara nyingi ndio hutokea, homa ya nyongo ya manjano si ya kawaida. Uvimbe wa mishipa ya damu katika retinali ni nadra katika ugonjwa huu.

Aina ya homa ya Q kimtazamo ni sawa na uvimbe ndani ya moyo (endocarditis) (), ambao unaweza kutokea miezi au miongo kufuatia maambukizi. Na ni hatari kama hutapapata tiba. Hata hivyo,kwa matibabu sahihi vifo hushuka mpaka karibu 10%.

Uonekanaji na Madhara

Homa Ya Q 
C. burnetii, homa y

Mdudu anapatikana sehemu zote isipokuwa New Zealand. Ulaya inaonekana kama hepatitis kuliko pneumonia kama ilivyo Marekani.

Bakteria hii ina uwezo wa kuhimili mazingira na ni hatari kwani moja tu anaweza kusababisha maambukizi. Njia ya kawaida ya maambukizi ni kuvuta pumzi ya vumbi iliyosindikwa, kugusa maziwa, nyama, sufi na hasa mazao ya uzazi yaliyosindikwa. Kupe anaweza kuhamisha kimelea kwa wanyama wengine. Uhamisho kati ya binadamu ni nadra sana na umeweza kuripotiwa katika kesi chache sana.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha wanaume wengi zaidi wameathirika kuliko wanawake, na hii inoonekana kutokana na aina mbalimbali za uwiano katika ajira.

"Walio katika hatari" ni pamoja, lakini si lazima, na:

  • wafanyakazi wa mifugo
  • wafanyakazi wa sehemu za kutunzia wanyama kabla ya kuuzwa.
  • wakulima
  • wakwangua manyoya
  • wasafirisha wanyama
  • wafanyakazi wa maabara ambao huchukua sampuli za mifugo au kutembelea sehemu za machinjio.
  • watu ambao hutenganisha na kuwatunza kangaroo
  • wafanyakazi wa (sehemu ya kuhifadhia mifugo) ambao hujifungia.

Utambuzi wa Ugonjwa

Utambuzi huzingatia vipimo vya kimiminika cha damu (kuangalia mwitikio wa vilindamwili ) kuliko kuangalia kiumbe chenyewe. Serology inaruhusu ugundulikaji wa maambukizi sugu pale viwango vya juu vya chembe ulinzi za mwili hupatikana dhidi ya maambukizi ya bakteria. Ugunduzi wa molekyulari ya DNA ya bakteria hutumika sana. Ukuzaji huwa ni mgumu na mara nyingi haupo katika maabara nyingi za kusomea wadudu wadogo.

Homa ya Q inaweza kusababisha endocarditis (maambukizo ya valvu za moyo ) ambayo inaweza kuhitaji acheokaridiografia transioesofageali kwa ajili ya uchunguzi. Homa ya manjano isababishwayo na homa ya Q hudhihirishwa na mwongezeko wa Alt na AST, lakini utambuzi yakinifu unawezekana kwa kuangalia tishu za ini ambazo huonesha athari kubwa kwenye viduara vya tishu vinavyosaidia damu kufunga {yaani fibrin ring granulomas}.

Tiba

Matibabu ya homa ya papo hapo ya Q kwa kutumia viuwavijidudu ni nzuri sana [onesha uthibitisho] na inapaswa kufanyika kwa kushauriana na mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza {/2. {3/} Madawa yatumikayo mara kwa mara ni doxycycline, Tetracycline, chloramphenicol, ciprofloxacin, ofloxacin, na hydroxychloroquine. Tatizo la muda mrefu ni vigumu kutibu na linaweza kuchukua hadi miaka minne ya matibabu na doxycycline na quinolone au doxycycline na hydroxychloroquine.

Wakati wa mimba,homa ya Q ni vigumu kutibu kwa sababu doxycycline na ciprofloxacin hutumika kwa nyakati tofauti wakati wa mimba. Matibabu yanayofaa huwa ni wiki tano kwa kutumia trimoxazole.

Kuzuia

Kinga inatolewa na Q-Vax, chanjo ya Australia iliyotengenezwa na kampuni ya CSL ambayo hufanya kiini kizima kisiweze kufanya kazi. . Chanjo ambayo hufanya kazi ndani ya ngozi huwa na Coxiella burnetii waliouawa. Ngozi na vipimo vya damu vinatakiwa kufanyika kabla ya chanjo kwa kutambua kinga iliyopo, sababu ni kwamba kuwachanja watu ambao tayari wanakinga kunaweza kusababisha athari kubwa ndani ya mwili. Baada ya dozi moja ya chanjo, kinga hueendelea kwa miaka mingi. Kupigwa chanjo tena huwa si lazima. Uchunguzi wa kila Mwaka unapendekezwa.

Mwaka 2001, Australia ilianzisha mpango wa kitaifa wa chanjo ya homa ya Q kwa watu wafanyao kazi katika maeneo ambapo ni rahisi kupata ugonjwa huu.

Umoja wa Urusi uliwahi kutengeneza chanjo ila madhara yake yalizuia utoaji wa leseni kwa ajili ya usambazaji wa dawa hiyo.

Vita vya kibiolojia

Homa ya Q imekuwa ikielezeka kuwa kama silaha ya kibaiolojia.

Marekani ilichunguza homa ya Q kama silaha yakibaiolojia katika miaka ya 1950 na baadaye kusanifishwa kama wakala OU. Pale Fort Detrick na Dugway Providing Ground majaribio ya kibinadamu yalifanywa kwa Whitecoat volunteers kutambua kipimo cha wastani (18 MICLD 50 / person i.h) na uendelevu wa maambukizi. Kama baiolojia sanifu,ilitengenezwa kwa wingi pale Pine Bluff Arsenal, kulikuwa na galoni 5,098 katika ghala ya silaha wakati wa kuzuia majeshi mwaka 1970.

Homa ya Q ni jamii ya kisababishi "B". Inaweza kuambukiza na ni stahimilivu katika usambaaji kwenye viwango mbalimbali vya joto. Vijidudu vya homa ya Q huweza kuishi kwenye ardhi hadi siku 60.

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

Homa Ya Q HistoriaHoma Ya Q MuonekanoHoma Ya Q Uonekanaji na MadharaHoma Ya Q Utambuzi wa UgonjwaHoma Ya Q TibaHoma Ya Q KuzuiaHoma Ya Q Vita vya kibiolojiaHoma Ya Q MarejeoHoma Ya Q Viungo vya njeHoma Ya QBakteriaBinadamuUgonjwaWanyama

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Tanganyika (maana)Kutoka (Biblia)Barua pepeHektariUkoloniKukiTulia AcksonMbaraka MwinsheheHali ya hewaNominoOrodha ya Marais wa KenyaHaki za watotoJose ChameleoneUkatiliMuda sanifu wa duniaBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaPumuUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaNduniNg'ombe (kundinyota)FalsafaTungo sentensiBabeliSiafuTume ya Taifa ya UchaguziSimuRufiji (mto)ViwakilishiUvimbe wa sikioKenyaMiundombinuMkoa wa RuvumaKiimboMchwaNdoaBibliaUchumiWaluguruHaki za wanyamaDuniaKiwakilishi nafsiSitiariMoses KulolaKisononoAla ya muzikiNgeliBikira MariaSaidi Salim BakhresaMaambukizi ya njia za mkojoPunyetoNdege (mnyama)TumbakuPijini na krioliWanyaturuVivumishi vya sifaMfuko wa Mawasiliano kwa WoteChama cha MapinduziBahashaKishazi huruUfugajiKiswahiliJinaJichoRupiaHistoria ya IranTaswira katika fasihiDiamond PlatnumzNileVivumishi vya kumilikiFutiMasafa ya mawimbiViwakilishi vya pekeeVivumishi vya idadi🡆 More