Ho Chi Minh

Ho Chi Minh, aliyezaliwa kwa jina Nguyễn Sinh Cung, (19 Mei 1890 - 2 Septemba 1969 ) alikuwa mwanasiasa wa chama cha Kikomunisti na kiongozi (waziri mkuu kutoka mwaka 1945 hadi 1955, na rais kutoka 1945 hadi 1969) wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam (Vietnam Kaskazini).

Ho Chi Minh
Ho Chi Minh mnamo mwaka 1946

Maisha ya awali

Jina la 'Hồ Chí Minh' alianza kulitumia wakati wa mapinduzi ya Agosti 1945. Alipozaliwa aliitwa Nguyễn Sinh Cung. Kulingana na desturi za Ukonfusio alibadilisha jina kuwa Nguyễn Tất Thành alipofikia umri wa miaka kumi. Baadaye alitumia majina bandia mbalimbali hasa kutokana na kazi yake ya kisiasa. Watu wa Vietnam mara nyingi humtaja kama Bác Hồ (Mjomba Ho).

Nguyen alizaliwa katika kijiji cha Kim Liên, kaskazini mwa Vietnam, wakati ule sehemu ya Annam iliyokuwa eneo la koloni la Ufaransa. Baba yake alikuwa hakimu. Nguyen alipokea mafunzo ya Kikonfusio akasoma baadaye kwenye shule ya Kifaransa.

Kuanzia mwaka 1911 hadi 1917 Nguyen alisafiri duniani akifanya kazi mbalimbali kwenye meli kama mpishi. Kwa vipindi vifupi alipata pia kazi katika miji ya Ufaransa, Marekani na Uingereza. Katika miaka 1919 hadi 1923 aliishi Paris ambako alijiunga na Wavietnam wengine katika kundi lililojadili madai ya uhuru kwa nchi yao. Alishiriki pia katika mikutano ya chama cha Kisoshalisti. Mwaka 1920 alijiunga na chama cha kikomunisti kilipojitenga na Wasoshalisti.

Mwaka 1923 alihamia Urusi alipoajiriwa na Komintern na kusoma kwenye chuo cha kikomunisti mjini Moscow.

Kati ya miaka 1924 hadi 1941 alitumwa na Komintern mara kadhaa kwenda China alipohusika kujenga chama cha Kikomunisti.

Kuunda Vietnam huru kwa vita dhidi ya Ufaransa

Mwaka 1941 Ho alirudi Vietnam iliyowahi kuvamiwa na Japani ingawa Wajapani waliruhusu Wafaransa kuendelea kutawala chini yao. Ufaransa iliyoshindwa na Ujerumani huko Ulaya ilidhoofishwa, na Wakomunisti Wavietnam walichukua nafasi kupigania uhuru. Ho aliunda vikosi vya wanamgambo wa Vietminh walioshambulia Wajapani na Wafaransa. Wakati Japani ilipaswa kusalimu amri kwenye mwaka 1945 na jeshi la Jamhuri ya China lilichukua nafasi ya Wajapani, wanamgambo wa Vietminh walitwaa mji wa Hanoi na kutangaza Jamhuri ya Vietnam na serikali iliyoongozwa na Ho Chi Minh.

Hata hivyo, kaskazini mwa Vietnam ilikuwa chini ya Jamhuri ya China iliyovumilia kuwepo kwa serikali ya Ho Chi Minh ambayo ilibaki bila mamlaka halisi.

Wakati Wafaransa waliporudi baada ya kupatana na China, Ho Chi Minh alikubali kubaki na Vietnam iliyojitawala chini ya ulezi wa Ufaransa. Lakini mwaka 1946 kulikuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa Vietminh na Wafaransa. Hapo Wafaransa walijaribu kurudisha hali ya kikoloni kamili. Hivyo vita ya Indochina ilianza.

Iliendelea hadi 1954 ambako jeshi la Vietminh ilishinda Wafaransa. Mapatano ya amani yaliacha kaskazini mwa Vietnam chini ya serikali ya Ho Chi Minh ilhali kusini kulikuwa chini ya serikali ya kaizari Bao Dai aliyesaidiwa na Marekani na Wafaransa waliokubali kumaliza utawala wao.

Vita ya Vietnam

Matokeo ya Vita ya Vietnam yalikuwa mgawanyiko wa nchi. Ho Chi Minh alitawala sasa sehemu ya kaskazini, ilhali Vietnam Kusini ilikuwa chini ya serikali iliyopinga Ukomunisti.

Hapo Ho pamoja na chama cha Kikomunisti waliamua kuanzisha makundi ya wanamgambo huko kusini ambao waliitwa Vietkong. Hao Vietkong walishambulia polisi na maafisa wa serikali ya kusini.

Marekani iliunga mkono Vietnam Kusini kwa msaada wa kijeshi, na Umoja wa Kisovyeti (ukiongozwa na Nikita Krushchev na kisha Leonid Brezhnev) na Jamuhuri ya Watu wa China (iliyoongozwa na Mao Zedong) iliendelea kuunga mkono juhudi za vita za Vietnam Kaskazini hadi ushindi wake.

Ho Chi Minh 
Kaburi la Ho Chi Minh mjini Hanoi

Kifo

Akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shida ya moyo, Hồ Chí Minh alijiuzulu na uongozi wa serikali na chama mnamo mwaka 1965. Kwenye asubuhi ya 2 Septemba 1969 alifariki baada ya shtuko la moyo.

Katika wosia wake aliandika alitamani kuchomwa na majivu yake yatawanywe kaskazini, katikati, na kusini mwa Vietnam. Walakini, chama kiliamua kuhifadhi mwili wake na kuuweka ndani ya kaburi ambapo unaoonyeshwa kwa wananchi na watalii wanaopewa nafasi kupita na kumwangalia.

Mnamo 1976, baada ya ushindi katika kusini, mji mkuu wa Vietnam Kusini, Saigon, ulipewa jina la Ho Chi Minh City kwa heshima ya kiongozi huyo.

Marejeo

Viungo vya Nje

Ho Chi Minh 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Ho Chi Minh 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Ho Chi Minh Maisha ya awaliHo Chi Minh Kuunda Vietnam huru kwa vita dhidi ya UfaransaHo Chi Minh Vita ya VietnamHo Chi Minh KifoHo Chi Minh MarejeoHo Chi Minh Viungo vya NjeHo Chi Minh189019 Mei1945195519692 SeptembaChama cha KikomunistiChama cha kisiasaJinaKiongoziMwakaMwanasiasaRaisVietnam KaskaziniWaziri mkuu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Steven KanumbaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaMikoa ya TanzaniaOrodha ya milima ya TanzaniaNathariMfumo wa upumuajiKupatwa kwa JuaMazingiraHedhiNomino za kawaidaMbaraka MwinsheheAbrahamuKinembe (anatomia)Ugonjwa wa uti wa mgongoHurafaMkoa wa TaboraKiongoziBunge la TanzaniaSitiariViwakilishi vya idadiMtume PetroEthiopiaUhuru wa TanganyikaMeno ya plastikiUfugajiNamba tasaTarbiaNdoa katika UislamuAdolf HitlerKenyaUsawa (hisabati)MbagalaSayariMkoa wa ShinyangaDaktariVichekeshoJava (lugha ya programu)Vidonda vya tumboDawatiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoRita wa CasciaIsraelOrodha ya milima mirefu dunianiUsafi wa mazingiraVivumishi vya -a unganifuSiasaHistoria ya WapareWajitaStephane Aziz KiUajemiBenjamin MkapaKisimaKiambishiSimuMuda sanifu wa duniaMizimuSaida KaroliUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaOrodha ya vitabu vya BibliaMbadili jinsiaMbooUandishiRaiaPijini na krioliKiboko (mnyama)BaruaHaitiBendera ya KenyaTungo sentensiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMkoa wa DodomaAustralia🡆 More