Waazeri (pia: Waazerbaijani, Waturuki wa Azerbaijan) ni watu wanaoongea lugha ya Kiazeri, wakazi hasa wa kaskazini-magharibi mwa Iran na nchi ya Azerbaijan.
Idadi yao hukadiriwa kuwa kati ya milioni 25 - 30; wengi wanaishi Iran (milioni 15) na Azarbaijan (milioni 9). Wachache wako pia Uturuki, Georgia na Armenia. Karibu wote ni Waislamu wa dhehebu la Shia.
Asili yao ni mchanganyiko wa mataifa na makabila mbalimbali. Watu wa maeneo ya Azerbaijan walikuwa wameanza kutumia Kiajemi kabla ya uvamizi wa Waarabu. Tangu karne ya 11 makabila ya Kituruki walipita hapa katika uhamisho wao kutoka Asia ya Kati kuelekea magharibi, wengi walibaki. Polepole wakazi walibadilisha tena lugha hadi Kiturki cha wageni kimekuwa lugha ya wananchi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Waazeri, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.