Rosaline Ufuoma Meurer (kuzaliwa 15 Februari 1992), ni mtayarishaji na mcheza filamu wa Nigeria, mzaliwa wa Gambia.
Anajulikana sana kwa uhusika wake katika filamu ya Oasis ya waka 2014 pamoja na uhusika wake kama Kemi Alesinloye katika filamu iliyoandaliwa na Ayo Makun kwa jina la Merry Men: The Real Yoruba Demons mwaka 2018.
Meurer alikulia nchini Gambia ambapo alipata elimu yake ya msingi. Ana astashahada ya usimamizi wa biashara na pia alisomea upigaji picha.
Katika umri wake mdogo, Meurer alipenda sana Ndege (uanahewa) na vyombo vya kupaa, alitamani aje kua mhudumu wa ndege au hata rubani. Alianza kazi kama mwanamitindo akiwa nchini Gambia, kabla ya kuhamia Nigeria mwaka 2009. Kipaji chake kilionekana na muigizaji na mwanasiasa Desmond Elliot akiwa Gambia mwaka 2009, ambaye alimshauri aanze kujaribu kuigiza nchini Nigeria. Alihamia Lagos, Nigeria na kuanza kazi ya kucheza filamu, alianza katika filamu ya Emem Isong kwa jina la Spellbound mwaka 2009, mwaka 2011 katika filamu ya In the Cupboard (film)|In the Cupboard.
Mwaka 2012, alihusika katika filamu ya Weekend Getaway. Baada ya uhusika wake katika filamu hiyo ya mwaka 2012, aliacha kazi ya uigizaji kwa muda na kurudi masomoni nchini Gambia, baadaye alirudi tena nchini Nigeria na kuendelea na kazi ya uigizaji. Aliporudi mwaka 2014, alikua miongoni mwa wahusika katika filamu ya Oasis, akiwa mhusika kwa jina la Kaylah. Mwaka uliofuatia, alicheza kama Nneka katika filamu ya Damaged Petal, alishiriki pia katika filamu ya Red Card na Open Marriage.
Mwaka 2017, alikua mhusika mkuu katika filamu ya Our Dirty Little Secret. Mwaka huohuo, alikua mhusika kwa jina la Monica katika maonyesho ya televisheni kwa jina la Philip and Polycarp alishiriki pia katika filamu ya The Incredible Father, Pebbles of Love na Our Dirty Little Secret. Baadaye aliachia filmu yake ya kwanza kwa jina la The Therapist's Therapy. Mwaka 2018, alihusika kama Valerie katika filamu ya Eniola Badmus kwa jina la Karma na pia aliigiza kama Kemi Alesinloye katika filamu ya Ayo Makun kwa jina la Merry Men: The Real Yoruba Demons.
Mnamo Mei 25 2017, Meurer aliongoza katika kukarabati mradi wa maji wa soko kuu ya Udu, Udu, Nigeria|Udu, jimbo la Delta. Kama balozi wa makanisa makubwa ya usimamizi wa wanawake na Watoto, alitoa msaada katika kliniki ya wanawake wajawazito na wazazi iliyopo Warri, jimbo la Delta.
Meurer ni balozi wa Multisheen Ebony. Mwaka 2015, aliteuliwa kua balozi wa “Big Church Foundation on Women and Child”. Alitokeza katika ukurasa wa mbele wa jarida la mwezi Aprili 2017 House Of Maliq Magazine. Mnamo Aprili 2019, alitia Saini ya idhini na DoctorCare247. Miezi minne baadae, alisaini idhini nyingine na Glo.
Meurer alizaliwa Gambia, baba yake ni mholanzi na mama yake anatokea jimbo la Delta nchini Nigeria. Ni mzaliwa wa kwanza katika familia yenye Watoto watatu.
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2009 | Spellbound | ||
2011 | In the Cupboard | ||
2012 | Weekend Getaway | ||
2015 | Damaged Petal | Nneka | |
2015 | Red Card | Kachi | |
2015 | Open Marriage | Becky | |
2016 | My Sister And I | ||
2017 | Pebbles of Love | Vanessa | |
2017 | Our Dirty Little Secret | Anita | |
2017 | The Incredible Father | Susan | |
2018 | Merry Men: The Real Yoruba Demons | Kemi Alesinloye | |
2018 | Karma | Valerie | |
2019 | Accidental Affair | Jenny | |
2020 | Circle of Sinners | Betty | |
TBA | Table of Men |
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2014 | Oasis | Kaylah | Mhusika mkuu |
2017 | Philip and Polycarp | Monica | Mhusika mkuu |
Mwaka | Tuzo | Kipengele | Matokeo | Rej |
---|---|---|---|---|
2017 | City People Movie Awards | Muigizaji bora wa kike chipukizi | mshiriki | |
La Mode Green | Tuzo maalumu ya utambuzi | Mshindi | ||
2016 | Nigeria Goodwill Ambassador Awards | Muigizaji bora ajae | Mshindi |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Rosaline Meurer, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.