Mnyoo-Unywele

Oda 2, familia 3

Mnyoo-unywele
Mnyoo-unywele (Gordius aquaticus)
Mnyoo-unywele (Gordius aquaticus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Ecdysozoa
Faila: Nematomorpha
Vejdovský, 1886
Ngazi za chini

  • Gordioidea Rauther, 1930
    • Chordodidae May, 1990
    • Gordiidae May, 1919
  • Nectonematoidea Rauther, 1930
    • Nectonematidae Ward, 1892

Minyoo-unywele ni spishi za minyoo-kuru za faila Nematomorpha zilizo ni ndefu na nyembamba sana kama nywele nene. Wapevu huishi huru katika maji matamu au ya chumvi na kuonekana mara nyingi kwenye hori za kunywea maji, mabwawa ya kuogelea, matangi ya maji, vijito na madimbwi. Lava ni vidusia wa arithropodi kama mbawakawa, mende, vivunjajungu, panzi, nyenje na gegereka.

Takriban spishi zote zina urefu wa mm 50-100, lakini baadhi yao ni ndefu zaidi hadi m 2. Unene wao ni mm 1-3. Minyoo-unywele wana kutikulo ya nje bila silio. Ndani ya mwili wana misuli inayopita kutoka mbele mpaka nyuma tu na utumbo usiofanya kazi bila mifumo ya kinyesi, upumuaji na mzunguko wa damu. Mfumo wa neva huwa na duara ya neva karibu na ncha ya mbele na kamba ya neva chini inayoenda kupitia mwili.

Minyoo hawa wana jinsia mbili tofauti na utungisho wa ndani wa mayai ambayo hutagwa kwa nyuzi za rojorojo. Wapevu wana gonadi za umbo la mcheduara zinazojifungua kwenye kloaka. Lava wana duara za ndoano za kutikulo na sindano kwenye ncha ya nyuma ambazo inaaminika kutumiwa kuingia katika vidusiwa. Wakiwa ndani ya kidusiwa, lava huishi ndani ya hemoseli na kunyonya virutubisho moja kwa moja kupitia ngozi yao. Maendeleo mpaka maumbile ya mpevu huchukua wiki au miezi na lava hubambua mara kadhaa wakikua.

Mnyoo-Unywele
Spinochordodes tellinii na kidusiwa wake Meconema thalassinum

Kwa Spinochordodes tellinii na Paragordius tricuspidatus, ambao wana panzi na nyenje kama vidusiwa wao, maambukizi huathiri ubongo wa kidusiwa. Hii husababisha mdudu kidusiwa kuruka ndani ya maji na kujizamisha na hivyo kurudisha mnyoo-unywele kwenye maji. P. tricuspidatus pia ana uwezo wa ajabu kustahimili kuliwa na mbuai kwa kidusiwa wao kwa kuwa na uwezo wa kunyanyuka kutoka kwa mbuai huyu. Kidusia huathiri macho ya Hierodula patellifera ili huyu avutiwe na nuru yenye uelekeo hususa. Kwa hivyo kidusiwa huingia ndani ya maji na mzunguko wa maisha wa kidusia hukamilika.

Picha

Kutazama

Minyoo-unywele katika nyenje

Marejeo

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya matajiri wakubwa WaafrikaKiboko (mnyama)Homa ya mafuaMenoViwakilishiDuniaShabaniUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaMtandao wa kijamiiSayansiDaftariWasukumaViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)ChuiDakuUkraineGKipanya (kompyuta)Kifo cha YesuAlomofuAzimio la kaziNgoziMkoa wa ArushaHuduma ya kwanzaWapareStadi za lughaDhahabuNgeli za nominoJakaya KikweteVivumishiAurora, ColoradoInternet Movie DatabaseSeli za damuUundaji wa manenoUfaransaKaswendeKabilaKilimanjaro (Volkeno)ChemchemiNembo ya TanzaniaKobeMkoa wa SongweNg'ombeWanyamweziUjerumaniKikohoziBenderaKaabaMoyoAgano la KaleGhubaKatekisimu ya Kanisa KatolikiKuraniParisMivighaUkoloni MamboleoSwalahKinuElimuDiniLugha ya kwanzaVivumishi vya ambaEverest (mlima)Kata za Mkoa wa Dar es SalaamMsokoto wa watoto wachangaWachaggaMkoa wa SingidaTeziUtandawaziMuzikiBurundiHali maadaKwaresimaBibliaPumuMungu ibariki AfrikaUgandaUfahamu🡆 More