Familia 16:
Kivunjajungu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kivunjajungu kijani wa Ulaya (Mantis religiosa) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
|
Vivunjajungu, vunjajungu au katamasikio ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Mantodea (mantis = nabii, eidos = umbo) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki na kusini (au kaskazini) kwa kanda za wastani. Kiwiliwili chao ni kirefu na chembamba. Miguu ya mbele imetoholewa kwa kukamata arithropodi wengine na hata vertebrata wadogo. Kwa kawaida koksa (coxa) za miguu ya wadudu ni fupi, lakini zile za miguu ya mbele ya vivunjajungu zimerefuka. Femuri na tibia zina miiba na meno inayowezesha mdudu kushika vizuri mawindo yake. Kama takriban wadudu wote vivunjajungu wana toraksi yenye sehemu tatu, lakini ile ya mbele, protoraksi, ni ndefu kuliko mbili nyingine pamoja na imeungwa vinamo na mesotoraksi. Hii inawezesha mdudu asogeze kichwa na miguu ya mbele pande zote wakati kiwiliwili kinatulia. Hata shingo ni kinamo na spishi kadhaa zinaweza kuzungusha kichwa kwa nyuzi 180.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kivunjajungu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kivunjajungu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.