Mtume Mathia (kwa Kigiriki Matthias kutokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake Zawadi ya Mungu) kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni mwaka 30 (au 33).
Mitume wa Yesu |
---|
|
Kabla ya Pentekoste wa mwaka huo, Mtume Petro alipendekeza kwamba mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na kura ya bahati ilimuangukia Mathia awe shahidi wa ufufuko wake.
Ingawa Biblia haina habari zaidi juu yake, inasemekana alifia dini na tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 14 Mei (Kanisa Katoliki na Anglikana), tarehe 9 Agosti (Waorthodoksi wa Mashariki) na tarehe 24 Februari (Walutheri na wengineo).
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Mathia kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mtume Mathia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.