Mpopi (kutoka Kiing.
Mpopi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Inakua hadi urefu wa mita 1 ikiwa na maua meupe, manjano na mara nyingi mekundu. Mpopi ni asili ya madawa ya kulevya ya afyuni na heroini yanayotumiwa pia kama madawa ya tiba hasa kwa kutuliza maumivu makali.
Mbegu zake hutumiwa kwa kutoa mafuta pia kama chakula ukichanganywa ndani ya keki na mikate.
Kemikali zinazosababisha matumizi ya afyuni ziko hasa katika utomvi wa mpopi lakini kwa kiasi kidogo pia kwenye majani na mbegu wake. Afyuni hutengenezwa kwa kukata tumba za ua la mpopi; utomvi mweupe unatoka nje na kuganda hewani kuwa masi kama mpira. Masi hii ni afyuni bichi.
Afyuni hulimwa hasa kwa ajili ya biashara haramu ya afyuni na heroini. Nchi yenye mashamba makubwa ni Afghanistan na Myanmar. Hata kama kilimo na biashara hii ni haramu wakulima maskini wanavutwa na mapato ambayo ni juu kuliko mapato kutokana na mazao ya chakula.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mpopi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.