Nusuoda 4:
Mdudu-koleo | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu-koleo (Anisolabis maritima) | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
|
Wadudu-koleo ni wadudu wadogo wa oda Dermaptera (derma = ngozi, ptera = mabawa) ambao wana serki kwa umbo wa koleo. Serki hizi hutumika kwa kushika mawindo, kwa kujitetea, kwa kukunja mabawa ya nyuma na wakati wa kujamiiana. Mabawa ya nyuma yakunjwa ili kufichwa chini ya yale ya mbele yaliyo mafupi.
Kuna spishi zinazoishi juu ya wanyama, lakini takriban spishi zote huishi nje na hula kila aina ya chakula: majani, maua, wadudu wadogo, maada ya mimea na wanyama waliokufa. Spishi kadhaa, kama mdudu-koleo wa Ulaya, zinaweza kuwa wasumbufu na kusababisha hasara katika mashamba. Lakini spishi nyingi zinasaidia wakulima kwa sababu wanakula wadudu wengine wasumbufu, kama vidukari.
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdudu-koleo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mdudu-koleo, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.