Laurenti Mfiadini

Laurenti (kwa Kilatini Laurentius; Valencia au Huesca, Hispania, 225 hivi - Roma, Italia, 10 Agosti 258) alikuwa shemasi mkuu wa Kanisa la Roma hadi alipouawa kwa kubanikwa kutokana na imani yake katika Yesu.

Laurenti Mfiadini
Laurenti mbele ya Valerianus.
Laurenti Mfiadini
Kifodini cha Mt. Laurenti kilivyochorwa na Tintoretto, Christ Church, Oxford, Uingereza.
Laurenti Mfiadini
Kifaa kinachosadikiwa kilitumika kumbanika Laurenti mjini Roma.
Laurenti Mfiadini
Jiwe ambapo maiti yake ililazwa huko Roma (San Lorenzo fuori le mura)
Laurenti Mfiadini
"Kifodini cha Mt. Laurenti" kilivyochongwa na Juan de León (1758). Kazi hii iko Real Academia de Bellas Artes de San Fernando, Madrid, Hispania.

Laurenti alikuwa msimamizi wa mali ya Kanisa la Roma iliyotumiwa kwa ajili ya kuwasaidia maskini. Serikali ya Kaisari Valerian iliwahi kumwua askofu wa Roma Sixtus II ikadai sasa Laurenti atoe hazina yote ya Kanisa kwa serikali ya Kaisari katika muda wa siku tatu. Laurenti alitumia muda huo kugawa pesa zote kwa maskini.

Akitamani kushiriki kifodini cha askofu wake, anavyosimulia Papa Leo I, siku alipotakiwa kufika mbele ya afisa wa serikali kukabidhi pesa alikuja pamoja na kundi kubwa la maskini, wagonjwa, walemavu, vipofu, wenye ukoma, wajane na mayatima. Halafu kwa dhihaka alimwambia akida, "Hao ndio hazina ya Kanisa". Akida alimtesa na kumfunga kwenye nondo za chuma juu ya moto hadi alikufa. Inasemekana ya kwamba Laurenti alivumulia mateso kimyakimya akisema mwishoni, "Ewe mtu maskini, kwangu moto huu umepoa lakini kwako utaleta maumivu ya milele". Alizikwa katika shamba la Mungu la Verano ambalo mpaka leo linaitwa jina lake.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu mfiadini, hasa siku ya kifodini chake.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Laurenti Mfiadini 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Laurenti Mfiadini  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Tags:

10 Agosti225258HispaniaImaniItaliaKanisa la RomaKilatiniRomaShemasiValenciaYesu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KinuArusha (mji)Ufufuko wa YesuIsraeli ya KaleRwandaMapenziWakingaUfaransaNyweleRohoBenjamin MkapaAntibiotikiHarmonizeMkoa wa GeitaKiambishi awaliMazingiraKukuFutariMaliasiliTaifaDiniMaishaKata za Mkoa wa Dar es SalaamUtendi wa Fumo LiyongoKamusi ya Kiswahili sanifuKamusi ya Kiswahili - KiingerezaViwakilishi vya sifaMkoa wa Dar es SalaamMuda sanifu wa duniaWanyamweziNgome ya YesuPumuMkoa wa Unguja Mjini MagharibiVipaji vya Roho MtakatifuUmoja wa MataifaMnyamaKaabaDakuMtakatifu PauloZakaAngkor WatDodoma (mji)JinaMeliMkoa wa MbeyaHistoria ya UislamuProtiniMkutano wa Berlin wa 1885IsraelMuundoDar es SalaamKishazi huruVitenziLilithInjili ya MathayoAli Hassan MwinyiDiplomasiaSemiTai (maana)SimbaAzimio la ArushaLahajaUandishiThenasharaAlasiriWaarabuMpira wa miguuNdovuVivumishi vya idadiPikipikiVAViwakilishi vya -a unganifuHeshimaMfumo wa upumuajiNomino za dhahaniaHuduma ya kwanzaMalawiMoroko🡆 More