Yatima (kwa Kiingereza orphan, kutoka Kigiriki ορφανός, orfanós) ni mtoto aliyefiwa au kutelekezwa moja kwa moja na wazazi wake wote.
Kwa kawaida mtoto aliyewapoteza wazazi wake wote wawili anaitwa yatima.
Watu wazima pia wanaweza kuitwa mayatima. Ingawaje, watu waliofikia utu uzima kabla wazazi wao hawajafariki kwa kawaida hawaitwi hivyo.
Kwa ujumla hili ni neno ambalo hutumika kuelezea watoto ambao wazazi wao walifariki kabla ya wao kufikia umri wa kujitegemea.
Watoto yatima mara nyingi huishi katika ukoo wa wazazi, katika nyumba ya yatima au kwa walezi. Katika nchi maskini pasipo mfumo mzuri wa nyumba za yatima kuna idadi kubwa ya mayatima wanaopaswa kuishi kwa kuombaomba au kutafuta riziki kwa kufanya kazi duni na hatari.
Kama yatima anaasiliwa na walezi anakuwa mtoto wao kisheria ingawa hali hii inaweza kuwa tofauti kulingana na sheria za nchi mbalimbali; hasa nchi nyingi za Kiislamu hazikubali mfumo wa kuasili kamili ila tu mfumo wa "kafala" ambayo ni aina ya ulezi ambapo mtoto anayepokelewa kisheria haitazamiwi kama mwanaukoo.
Vitabu mbalimbali vya dini, vikiwemo vile vya Biblia na Kurani , vinasema sana kuhusu watoto yatima ili kutetea haki zao na kuhimiza huruma kwao. Muhammad mwenyewe alikuwa yatima.
Mayatima si wengi katika nchi zilizoendelea, lakini ni wengi katika nchi zinazoendelea au zenye vita.
Bara | Idadi ya mayatima (mara elfu) | Asilimia zao kati ya watoto wote |
---|---|---|
Afrika | 34,294 | 11.9% |
Asia | 65,504 | 6.5% |
Amerika ya Kilatini na Karibi | 8,166 | 7.4% |
Jumla | 107,964 | 7.6% |
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Yatima, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.