Hifadhi Ya Taifa Ya Ziwa Nakuru: Hifadhi ya taifa nchini Kenya

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru ni mbuga ya wanyama nchini Kenya iliyoko kando ya Ziwa Nakuru, karibu na mji wa Nakuru.

Umbali wa Nairobi ni km 140. Geti kuu liko kilomita 4 kutoka mji wa Nakuru. Eneo lake ni takriban km² 188. Inajulikana hasa kwa wingi wa ndege aina ya heroe na kundi la vifaru ambao wanaonekana hapa kwa uhakika mkubwa kulingana na mbuga nyingine za Kenya.

Hifadhi Ya Taifa Ya Ziwa Nakuru: Hifadhi ya taifa nchini Kenya
Eneo la mbuga kando la Ziwa Nakuru
Hifadhi Ya Taifa Ya Ziwa Nakuru: Hifadhi ya taifa nchini Kenya
Ndege za Heroe ziwani

Mbuga ilianzishwa mwaka 1961. Sababu ya kuianzisha ilikuwa idadi kubwa ya ndege wa heroe wanaokusanyika hapa. Wakati mwingine huhesabiwa kuwa hadi milioni mbili. Idadi ya heroe hubadilika kimajira kulingana na kiasi cha algae ambazo ni chakula chao hasa.

Baadaye vifaru walipelekwa hapa wakati walivindwa ovyo katika mbuga nyingine nchini na kuwa hatarini mwa kupotea. Leo hii kuna takriban vifaru 60 mbugani wanaolindwa na walinzi wa pori. Hadi leo watoto yatima wa vifaru wanaopatikana katika mbuga mbalimbali wanapelekwa hapa. Vilevile kama hali ya uwindaji ovyo unazidi katika eneo fulani na walinzi walishindwa kuukomesha vifaru walitiwa sindano ya kuwatuliza, kukamatwa na kupelekwa Nakuru. Kutokana na hali ya kuhatarishwa kwa vifaru mbuga yote imezungukwa na fensi.

Nje ya vifaru kuna takriban spishi 56 za mamalia mbalimbali pamoja na spishi 450 za ndege.

Marejeo


Viungo vya nje

Tags:

HeroeKenyaKifaruKm²KundiMbugaNairobiNakuruNdege (mnyama)UmbaliWanyamaZiwa Nakuru

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

IndonesiaMkopo (fedha)Historia ya TanzaniaBruneiPijini na krioliOrodha ya kampuni za TanzaniaMkoa wa KigomaVirusi vya UKIMWIHistoria ya ZanzibarMaadiliMadiniOrodha ya viongoziWabunge wa Tanzania 2020Ng'ombe (kundinyota)Ziwa ViktoriaSentensiLakabuMkoa wa MbeyaMadawa ya kulevyaMatumizi ya lugha ya KiswahiliLady Jay DeeNuktambiliKiboko (mnyama)SexKisukuruUandishiUKUTAAdolf HitlerMwanza (mji)Diamond PlatnumzLahaja za KiswahiliMajina ya Yesu katika Agano JipyaPasakaMkoa wa RukwaMkoa wa NjombeKiarabuNg'ombePasifikiVisakaleNyukiInshaUchaguziMwanaumeKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniKifua kikuuWahayaUnyevuangaMkoa wa LindiBendera ya ZanzibarAnwaniMafumbo (semi)Ukwapi na utaoOrodha ya milima ya TanzaniaUkristoMr. BlueMjombaMuda sanifu wa duniaWaziriVitamini CMkoa wa PwaniTabianchiMbuga za Taifa la TanzaniaSarufiKishazi huruWahadzabeDhima ya fasihi katika maishaMajeshi ya Ulinzi ya KenyaDaktariKifaru🡆 More