Kigong'ota

Jenasi 27; spishi 32 katika Afrika:

Kigong'ota
Kigong'ota mkia-njano
Kigong'ota mkia-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Piciformes (Ndege kama vigong'ota)
Familia: Picidae (Ndege walio na mnasaba na vigong'ota)
Nusufamilia: Picinae (Ndege walio na mnasaba sana na vigong'ota)
Ngazi za chini

  • Blythipicus Bonaparte, 1854
  • Campephilus G.R. Gray, 1840
  • Campethera G.R. Gray, 1841
  • Celeus Boie, 1831
  • Chloropicus Malherbe, 1845
  • Chrysocolaptes Blyth, 1843
  • Colaptes Vigors, 1825
  • Dendrocopos Koch, 1816
  • Dendropicos Malherbe, 1849
  • Dinopium Rafinesque, 1814
  • Dryobates Boie, 1826
  • Dryocopus Boie, 1826
  • Gecinulus Blyth, 1845
  • Geocolaptes Swainson, 1832
  • Hemicircus Swainson, 1837
  • Hypopicus Bonaparte, 1854
  • Meiglyptes Swainson, 1837
  • Melanerpes Swainson, 1832
  • Mulleripicus Bonaparte, 1854
  • Picoides Lacépède, 1799
  • Piculus Spix, 1824
  • Picus Linnaeus, 1758
  • Reinwardtipicus Bonaparte, 1854
  • Sapheopipo Hargitt, 1890
  • Sphyrapicus S.F. Baird, 1858
  • Veniliornis Bonaparte, 1854
  • Xiphidiopicus Bonaparte, 1854

Vigong'ota, gongonola, gogota, vigotagota au ving'ota ni ndege wa nusufamilia Picinae katika familia Picidae. Ni bora kutengea spishi za nusufamilia Picumninae jina “kigogota”. Inawakilishwa katika Afrika na kigogota wa Afrika. Vigong'ota vinatokea misituni na maeneo mengine yenye miti kila mahali pa dunia isipokuwa Madagaska, Australia, New Zealand na kanda za Aktiki na Antaktiki.

Spishi nyingi ni nyeusi mgongoni kwenye madoa na/au mabaka meupe au njano. Spishi nyingine zina rangi ya majani au kahawa. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Mkia una manyoya shupavu na umsaidia ndege kutembea wima mashinani kwa miti. Ndege hawa wana domo lenye nguvu ambalo hutumia kugogota miti na kutafuta wadudu katika nyufa za miti. Ulimi wao mrefu wa kunata na wenye nywele uwasaidia kuwatoa wadudu. Zaidi ya wadudu vigong'ota hula matunda na makokwa; spishi nyingine hula hata utomvu wa miti. Dume huchimba tundu katika mti na pengine jike amsaidia. Huyu huyataga mayai 2-6 ndani ya tundu.

Spishi za Afrika

Jenasi za mabara mengine

Picha

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Daudi (Biblia)Nguzo tano za UislamuOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaUfugaji wa kukuZana za kilimoSanaa za maoneshoMongoliaMjasiriamaliUaFamiliaVidonda vya tumboVasco da GamaSheriaZakaUtafitiShairiTmk WanaumeNguruweIndonesiaMjombaDini nchini TanzaniaNelson MandelaHistoria ya WapareSayansiOrodha ya nchi za AfrikaVivumishi vya -a unganifuMzabibuNairobiVivumishi vya sifaKifua kikuuMkungaAnna MakindaZuchuDhima ya fasihi katika maishaKaabaSaida KaroliKiambishi awaliSinagogiFasihiMethaliDar es SalaamMusaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaVivumishi vya idadiUtapiamloTamathali za semiKata za Mkoa wa Dar es SalaamKipindi cha PasakaTwigaBahari ya HindiSikioNomino za pekeeNominoWasafwaMbogaWallah bin WallahPasaka ya KiyahudiKamusi elezoNimoniaBunge la Afrika MasharikiWazaramoHifadhi ya SerengetiBaraza la mawaziri TanzaniaManchester CityVipaji vya Roho MtakatifuMkoa wa SingidaMzeituniOrodha ya Marais wa BurundiMatendeDhamiriTarakilishiMkoa wa Unguja Mjini MagharibiTanzaniaKihusishiMuundo wa insha🡆 More