Kiev

Kiev (pia:Kyiv - Kiukraine: Київ) ni mji mkuu wa Ukraine na pia mji mkubwa wa nchi hii wenye wakazi milioni mbili.

Iko kando la mto Dnepr kwa 50°27′00″N, 30°31′24″E.

Kiev
Mahali pa Kiev nchini Ukraine

Historia

Kiev inaaminiwa iliundwa mnamo ya karne ya 6 BK. Iliendelea kuwa mji mkuu wa Rus iliyokuwa milki kubwa ya kwanza ya Waslavoni ya mashariki. Mtemi Mkuu Vladimir I aliamua kupokea Ukristo akaamuru wakazi wote kubatizwa mtoni mara moja. Katika kumbukumbu la Ukraine na Urusi hii ilikuwa chanzo cha utamaduni wa kiorthodoksi wa Waslavoni ya mashariki. Hivyo Kiev inaitwa "mji mama wa miji yote ya Urusi".

Tar. 6 Desemba 1240 Kiev ilitekwa na jeshi la Wamongolia na kuchomwa moto. Mji ukafufuka tena lakini ukaendelea kuwa mji mdogo na makao makuu ya jimbo la Ukraine chini ya nchi mbalimbali zilizotawala yehemu hiyo kama Poland au Urusi.

Kiev ikaanza kukua na kuwa mji mkubwa wa tatu wa Milki ya Urusi katika mapinduzi ya viwandani ya karne ya 19. Baada ya mapinduzi ya Kibolsheviki ikawa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Kiev iliharibiwa vibaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikajengwa upya na kukua. Ajali ya kinyuklia ya Chernobyl ilitokeea karibu na mji lakini haikuuathiri sana kwa sababu upepo ulipeleka mavumbi ya sumu upande mwingine. Tangu uhuru wa Ukraine mwaka 1991 mji mkuu wa nchi hii.

Picha za Kiev

Kiev  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kiev kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Anwani ya kijiografiaKiukraineMji mkuuUkraine

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Bonde la Ufa la Afrika ya MasharikiAli KibaMkoa wa Dar es SalaamMkutano wa Berlin wa 1885Ugonjwa wa kuharaLugha za KibantuUtataMkunduKataAthari za muda mrefu za pombeMikoa ya TanzaniaUmoja wa AfrikaBungeTarbiaMvua ya maweAmri KumiWilaya ya Unguja Magharibi AMkoa wa DodomaWamasaiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaUaminifuMnyoo-matumbo MkubwaMasadukayoUhuru wa TanganyikaAfrikaMsamahaZiwa ViktoriaOrodha ya makabila ya TanzaniaVita ya uhuru wa MarekaniKamusiUongoziKisaweElimu ya bahariMpira wa kikapuMpwaViwakilishi vya kuoneshaKaswendeMbadili jinsiaManchester United F.C.LughaMajigamboMaudhui katika kazi ya kifasihiFasihiIsimujamiiOrodha ya nchi kufuatana na wakaziNyangumiOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaSomo la UchumiSeli za damuWasukumaChuo Kikuu cha DodomaTetemeko la ardhiMuundoMlima wa MezaUtumwaSimba (kundinyota)NdovuMohammed Gulam DewjiSelemani Said JafoIsimilaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniHekimaTetekuwangaHedhiMbuInshaAkiliVasco da GamaDola la RomaAfande SeleWilaya ya Ilala🡆 More