Vladimir Mkuu (958 hivi – 15 Julai 1015) alikuwa mtemi wa Kiev na Novgorod kuanzia mwaka 980 hadi kifo chake.
Mwaka 988 alipokea ubatizo kutoka kwa mapadre wa Kanisa la Bizanti uliofuatwa na ubatizo wa familia na wananchi wa utemi wake aliojitahidi kwa nguvu zote kuwaleta kwenye imani ya Kikristo .
Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni wa Urusi, Ukraina na Belarus pamoja na historia yote iliyofuata, kwa kuwa Kanisa la Kiorthodoksi liliendelea kuwa dini rasmi katika milki za Kirusi hadi Mapinduzi ya Urusi ya 1917.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Vladimir Mkuu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.