Fibonacci (mnamo 1175 - 1250) alikuwa mtaalamu wa hisabati kutoka nchini Italia.
Anakumbukwa kama mwanahisabati muhimu zaidi wa Ulaya wakati ya zama za kati.
Jina lake la kiraia ilikuwa Leonardo wa Pisa lakini aliitwa kwa jina la baba yake Bonacci.
Fibonacci anakumbukwa hasa kwa jedwali la namba linaloitwa mfululizo wa Fibonacci.
Linaanza hivi: 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21, 34, 55, 89, ...
Katika mfululizo huu namba inayofuata ni jumla ya namba mbili zinazotangulia:
1 + 1 = 2 1 + 2 = 3 2 + 3 = 5 3 + 5 = 8 5 + 8 = 13 8 + 13 = 21 13 + 21 = 34 21 + 34 = 55 34 + 55 = 89 55 + 89 = 144 89 + 144 = 233 144 + 233 = 377 233 + 377 = 610 377 + 610 = 987 610 + 987 = 1597 987 + 1597 = 2584 na kadhalika...
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Fibonacci, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.