Etimolojia

Etimolojia (kutoka gir.

Maneno pamoja na matamshi na tahajia hubadilika polepole. Yanaweza kuunganishwa au kufupishwa. Maneno huhamia kutoka lugha moja hadi nyingine na hapo yanaweza kubadilisha maana. Maneno mapya yanabuniwa kwa vitu vipya visivyojulikana awali.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu na hapo asili ya maneno mengi inaweza kutambuliwa kwa kulinganisha lugha mbalimbali ya Kibantu. Lakini Kiswahili ni pia lugha iliyopokea maneno mengi kutoka nje, hasa kutoka Kiarabu, baadaye kutoka Kireno na lugha za Kihindi na siku hizi kutoka Kiingereza. Ilhali lugha hizi zimepokea pia maneno kutoka asili nyingine wakati mwingine historia ya neno ni kama safari katika historia ya kibinadamu.

Mifano kadhaa

  • "Etimolojia" imefika katika Kiswahili kutoka Kiingereza etymology lakini kiasili ni neno la Kigiriki cha Kale lililoundwa kuotokana maneno ya ἔτυμον etimon ("maana ya kweli") na -λογία -logia ("somo la..", "elimu kuhusu"). Neno hili la Kigiriki lilipokelewa katika Kilatini ambacho baadaye kilikuwa lugha ya elimu katika Ulaya ya MAgharibi wa karne nyingi na hivyo kuingia katika lugha nyingi za Ulaya.
  • Kitabu ina asili ya Kiarabu ( كتاب, kitabun); inaonekana ni wafanyabiashara Waislamu waliotumia lugha ya Kiarabu waliopeleka kitu hiki katika mazingira yasiokuwa na maandishi kwa hiyo neno la kigeni likapokelewa moja kwa moja kwa kitu kigeni.
  • Samaki pia ni neno lenye asili ya Kiarabu (سمك samakun); bila shaka wenyeji wa Uswahilini walikuwa na neno la Kibantu kwa samaki na hapa kuna swali kwa nini waliaacha neno lao la kiasili kwa neno la nje; kuna hoja ya kwamba kule pwani samaki zilikuwa vyakula vilivyouzwa na wenyeji kwa wageni waliofika kwa jahazi na hivyo waliona faida wakitumia lugha ya wateja.
  • Muhindi kama jina la nafaka linatunza uhusiano na Uhindi ingawa uwzekano mkubwa ni imefika Afrika kutoka Amerika kupitia Wareno na Wahispania. Katika lugha za Ulaya mara nyingi iliitwa "nafaka ya Uhindi" (ing. Indian corn, far. ble de Inde) kwa sababu Kolumbus aliamini ya kwamba alifika Uhindini ya Asia na Wahispania pamoja na Wareno waliita nchi walizotawala katika Amerika "India" kwa karne zilizofuata. Hata hivyo kuna uwezekano ya kwamba nafaka hii ilifika pia kutoka Bara Hindi moja kwa moja kwa sababu kuna uwezekano ya kwamba ilijulikana pale kabla ya Kolumbus . Inawezekana pia ya kwamba wenyeji wa pwani walitunga jina hilikwa kudokeza ni nafaka kutoka sehemu za mbali.
  • Maneno kama Tanzania, UKIMWI au BAKITA yametungwa juzijuzi tu kwa unganisha sillabi ya majina mengine: TANganyika na ZANzibar kuwa Tanzania, Uhaba wa KInga MWIlini kuwa Ukimwi, BAraza ya KIswahili TAnzania kuwa Bakita.

Kamusi

Kwa lugha nyingi kuna kamusi za pekee zinazoonyesha etimolojia ya maneno. Kati ya Kamusi za Kiswahili hadi sasa hakuna kamusi ya etimolojia hasa.

  • Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI inadokeza kwa kifupi lugha asilia kama neno la Kiswahili lina asili kwa lugha ya nje.
  • Standard Swahili-English Dictionary ya Madan-Johnson inataja asili ya maneno kwa kirefu zaidi kiasi
  • Kamusi ya Kiswahili - Kifaransa iliyotolewa na Charles Sacleux mwaka 1939 hadi sasa ina maelezo bora na pana ya etimolojia ya maneno ya Kiswahili - lakini inatoa maana kwa Kifaransa tu.

Marejeo

Viungo vya Nje

Kujisomea

  • Skeat, Walter W. (2000). The Concise Dictionary of English Etymology, repr ed., Diane. (ISBN 0-7881-9161-6)
  • Skeat, Walter W. (1963). An Etymological Dictionary of the English Language. (ISBN 0-19-863104-9)
  • Snoj, Marko (2005). Etymology. In: Strazny, Philipp (ed.). Encyclopedia of Linguistics. New York: Fitzroy Dearborn, vol. 1: A–L, pages 304–306.
  • C. T. Onions, G. W. S. Friedrichsen, R. W. Burchfield, (1966, reprinted 1992, 1994). Oxford Dictionary of English Etymology. (ISBN 0-19-861112-9)
  • Liberman, Anatoly (2005). "Word Origins...and How We Know Them: Etymology for Everyone." (ISBN 0-19-516147-5)
  • Zuckermann, Ghil'ad (2003). Language Contact and Lexical Enrichment in Israeli Hebrew. Palgrave Macmillan. ISBN 1-4039-1723-X. 
  • Hayakawa, Isamu, (2014). A Historical Dictionary of Japanese Words Used in English. Revised and Corrected Edition. Amazon (Tokyo: Texnai).

Tags:

Etimolojia Mifano kadhaaEtimolojia KamusiEtimolojia MarejeoEtimolojia Viungo vya NjeEtimolojia KujisomeaEtimolojiaGir.Ing.

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MaadiliJose ChameleoneMahakamaDuniaViwakilishiMpira wa miguuChama cha MapinduziJumuiya ya MadolaDiniOrodha ya Magavana wa TanganyikaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiMandhariSanaaVivumishi vya urejeshiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaOrodha ya majimbo ya MarekaniMajigamboHekalu la YerusalemuUzazi wa mpango kwa njia asiliaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuNguruweHadithiRitifaaKata za Mkoa wa MorogoroSakramentiMitume wa YesuKipindupinduUvimbe wa sikioMilanoUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMwanaumeUajemiAgano la KaleOrodha ya Marais wa TanzaniaMkoa wa Dar es SalaamNdoaMilaMahindiBidiiBawasiriMshororoOrodha ya viongoziMagharibiUandishi wa inshaRamaniUmememajiSaidi Salim BakhresaShengWingu (mtandao)Mkopo (fedha)MamaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarAli KibaWhatsAppJinaNg'ombeKinembe (anatomia)IntanetiLeonard MbotelaKisimaFasihi andishiFigoVita Kuu ya Pili ya DuniaWimboTanganyika African National UnionDar es SalaamKoloniInstagramHomoniPesaHistoria ya Uislamu🡆 More