Mashua

Mashua ni jina la jumla la vyombo vya kusafiri kwenye maji.

Zinaweza kuendeshwa kwa njia mbalimbali, kama makasia, matanga na injini. Mashua zenye injini huitwa boti kwa kawaida na zilizo kubwa sana huitwa meli. Ikiwa injini inafanya kazi kwa mvuke, mashua inaitwa merikebu.

Mashua
Mashua karibu na Lamu
Mashua
Jahazi karibu na Doha
Mashua
Boti la polisi huko Venezia, Italia.
Mashua
Boti la kuokolea uhai huko Ufalme wa Muungano.

Mashua hutengenezwa kwa maada mbalimbali, kama mbao, mafunjo, plastiki au feleji. Zinasafiri kwenye bahari, maziwa na mito, na kubeba watu au mizigo au yote. Mashua ambazo hutumiwa kuvuka mito huitwa feri au vivuko. Zile zinazoweza kwenda chini ya maji huitwa manowari.

Huko pwani ya Afrika ya Mashariki, aina mbili za mashua kubwa kiasi za mbao zenye (ma)tanga ni za kawaida. Jahazi ndilo kubwa zaidi na linatumika kwa biashara katika pwani na kuelekea Uarabuni na Uhindi. Mashua hapa ni chombo kidogo zaidi cha mbao ambacho hutumiwa mara nyingi kwa uvuvi. Aina hizi zote mbili zimejengwa kwa miunda ya mbao.

Aina nyingine mbili za mashua zimetengenezwa kwa magogo ya miti yaliyotemuliwa. Sahili zaidi ni mtumbwi, unaotumika karibu na pwani na kwenye komeo za bahari na mito. Unasukumwa kwa kafi au upondo. Kwa ujumla huwa na urefu wa m 2 au 3 lakini unaweza kuwa hadi m 6. Mitumbwi midogo inaitwa hori na hutumika kwa usafiri kati ya ufuko na mashua kubwa zaidi.

Aina nyingine ni ngalawa, ambayo ni kubwa kuliko mtumbwi. Ingawa awali zilitengenezwa kutoka kwa gogo kubwa la mti, sasa mara nyingi hutengenezwa kwa mbao. Kwa kawaida hubeba tanga. Inatofautishwa na mashua kwa gubeti yake iliyoinuliwa na shetri iliyochongoka (mashua ina shetri ya mraba).

Marejeo

Viungo vya nje

Mashua 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


Mashua  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mashua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BotiInjiniMajiMeliMerikebuMvukeTanga

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WangoniHadhiraRisalaJohn MagufuliFamiliaUsafi wa mazingiraKipindupinduUandishi wa barua ya simuC++MuhimbiliUturukiGoba (Ubungo)MperaAlizetiUnyevuangaUislamuMsitu wa AmazonMungu ibariki AfrikaTanganyika (ziwa)Lugha ya taifaTanganyika (maana)Uzazi wa mpangoUchawiJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUDANevaMwakaAlama ya barabaraniMtandao wa kijamiiWapareOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaNusuirabuMkunduKiambishiMjombaWaziriClatous ChamaMbagalaMmeaMvuaJoyce Lazaro NdalichakoSayansi ya jamiiElimuUgonjwa wa kuharaBikira MariaMkoa wa KigomaMuhammadOrodha ya Magavana wa TanganyikaMajiVirusi vya CoronaKiarabuMbeya (mji)Aina za manenoMoscowNabii EliyaMichael JacksonOrodha ya milima ya AfrikaDar es SalaamWaheheMbwana SamattaSikioUajemiSitiariWachaggaWarakaKitenzi kikuu kisaidiziUpendoMbuniUpepoEe Mungu Nguvu YetuDamu🡆 More