Yesu kuzaliwa na Bikira ni fundisho la imani linalosema kuwa Yesu Kristo alitungwa tumboni mwa mama yake, Bikira Maria, kwa uwezo wa Mungu (Roho Mtakatifu) tu, na kuwa Maria alipomzaa alikuwa bado bikira.
Katika Biblia ya Kikristo fundisho hilo linapatikana katika Injili mbili zilizo tofauti hata kwa vyanzo katika uzazi na utoto wa Yesu: Math 1:18-25 na Lk 1:26-38.
Mathayo anathibitisha hilo kwa kutaja utabiri wa maneno ya Isa 7:14 katika tafsiri ya Kigiriki ya Septuaginta: "Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana, nao watamwita jina lake Emmanuel, yaani Mungu pamoja nasi".
Fundisho hilo linashikiliwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.
Hata Waislamu wanakubali fundisho hilo kutokana na Kurani, hasa sura 3 (Al Imran) na 19 (Maryam (sura)).
Mara nyingine fundisho hilo linachanganywa na mengine tofauti, kama vile utakatifu usio na doa wa Mariana ubikira wa kudumu aliokuwa nao maisha yake yote
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yesu kuzaliwa na Bikira kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Yesu kuzaliwa na Bikira, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.