Wamormoni

Wamormoni ni kundi la watu wanaohusiana na dini ya Mormoni, iliyoanzishwa na Joseph Smith huko New York, Marekani, katika miaka ya 1820 akidai alipata njozi na kuonyeshwa kitabu kitakatifu.

Wamormoni
Kioo cha rangi kikionyesha njozi ya kwanza ya Joseph Smith.

Baada ya kifo chake (1844), Wamormoni walimfuata Brigham Young hadi eneo la Utah.

Leo wengi wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku ya Mwisho (kifupisho cha Kiingereza LDS Church).

Kiini cha utamaduni wao ni jimbo la Utah, ambapo wao ndio wengi kati ya wakazi wote, lakini siku hizi Wamormoni wanaoishi nchini Marekani ni wachache kuliko wanaoishi nje kutokana na umisionari mkubwa wanaoufanya duniani kote.

Idadi yao inakadiriwa kuwa milioni 15.

Imani yao

Wamormoni 
Mpango wa Wokovu.

Wamormoni wanasadiki Biblia pamoja na maandishi mengine kama vile Kitabu cha Mormoni.

Wanasisitiza sharti la kumfuata Yesu Kristo ili kumrudia Mungu, pamoja na kupata ubatizo.

Wamormoni wanajiita Wakristo, ingawa mafundisho yao mbalimbali ni tofauti na yale ya madhehebu yote ya Ukristo, kiasi cha kutokubaliwa nayo (k.mf. Kanisa Katoliki halitambui ubatizo wao, hivyo linawahesabu kama dini tofauti).

Maadili

Pamoja na kukubali mitara kwa msingi wa Agano la Kale, Wamormoni wana maadili imara upande wa jinsia (wakipinga uasherati, uzinifu na ushoga) na wa matumizi ya mwili (vileo, tumbaku, kahawa, chai n.k.).

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wamormoni  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Wamormoni Imani yaoWamormoni MaadiliWamormoni TanbihiWamormoni MarejeoWamormoni Viungo vya njeWamormoniDiniJoseph SmithKitabuMarekaniMiaka ya 1820New YorkNjozi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Cristiano RonaldoOrodha ya Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoVivumishi vya kuoneshaUmoja wa AfrikaNdoa katika UislamuMichael JacksonKobeSayari ya TisaMofolojiaOrodha ya viongoziZuchuChombo cha usafiriMlo kamiliSanaaWanyama wa nyumbaniLionel MessiKwaresimaDayolojiaOrodha ya nchi za AfrikaHoma ya matumboOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaKatibaThabitiPasaka ya KiyahudiBara ArabuAmfibiaHektariLenziLisheVivumishi vya pekeeMaajabu ya duniaUlemavuDZakaNetiboliMahindiWAli Hassan MwinyiDaftariKinyongaJulius NyerereMwislamuMjasiriamaliMji mkuuMbeguRafikiMziziKengeHadhiraDiniMsamiatiNairobiJinaMbeya (mji)Kata za Mkoa wa MorogoroErling Braut HålandLugha ya kigeniKaswendeVielezi vya mahaliBawasiriUgonjwa wa kuharaBongo FlavaWilaya za TanzaniaGesi asiliaJamhuri ya Watu wa ChinaHekaya za AbunuwasiBob MarleyRohoChombo cha usafiri kwenye majiSiasaMtawaUtoaji mimbaDiego GraneseVita ya Maji MajiNikki wa PiliKuchaKipandausoUsawa (hisabati)Ubongo🡆 More