Nusufamilia 2, jenasi 9 za tumbusi:
Tumbusi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tumbusi uso-njano | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
|
Tumbusi au tai mzoga ni ndege wakubwa wa nusufamilia Aegypiinae na Gypaetinae katika familia Accipitridae ambao hula mizoga. Wana mnasaba na tai. Huko Amerika kuna ndege wafananao na tumbusi, lakini wale hawana mnasaba sana na huwekwa katika familia Cathartidae. Tumbusi huvumbua mizoga kwa macho, lakini wale wa Marekani wananusa vizuri pia.
Spishi nyingi za tumbusi zina kichwa bila manyoya. Sifa bainifu hii imekua kuzuia manyoya ya kichwa yasichafuliwe kwa damu wakati tumbusi akiingiza kichwa chake ndani ya mzoga. Kichwa chenye upara kinaweza kusafishwa kwa urahisi ndani ya mto au ziwa.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Tumbusi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.