Trafiki

Trafiki ni jumla ya watumiaji wa njia za usafiri, hasa barabara, kama vile magari, mabasi, malori, waenda kwa miguu na mikokoteni.

Ni pia jina la askari maalumu anayesimamia usalama barabarani. Mtandaoni, neno trafiki lina maana ya idadi ya watumiaji wanaotembelea tovuti.

Trafiki
Trafiki Gwalior, India

Matumizi

Nchini Kenya neno "trafiki" hutumika kumaanisha jumla ya watumiaji wa njia ya usafiri. Kwa mfano, Idara ya Trafiki ya polisi, sheria za trafiki na maafisa au polisi wa trafiki.

Nchini Tanzania, neno "trafiki" hutumika kama kuwa rejelea askari wa usalama barabarani.

Sheria za trafiki

Sheria za trafiki au pia sheria za barabarani ni sheria na taratibu zinazofuatwa ili kudumisha usalama kwa manufaa ya watumiaji wote wa barabara. Sheria msingi za barabarani zimeelezwa katika mkataba wa kimataifa, Mkataba wa Vienna wa Trafiki Barabarani wa mwaka 1968 ulio chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Kimsingi, mataa ya trafiki yanafaa kuzingatiwa, waenda kwa mguu wanafaa kupatia magari njia isipokuwa katika kivuko cha milia, waenda kwa mguu wanafaa kuwa makini wanapovuka barabara na magari yanafaa kutumia upande wa kuendeshea kulingana na sheria za nchi.

Kila nchi ina sheria msingi za barabarani. Serikali za mashinani kama zile za miji na kaunti zinaweza kuongezea kulingana na mahitaji yake. Sheria ya trafiki ya Kenya (kwa Kiingereza: Traffic Act Archived 13 Julai 2019 at the Wayback Machine.) ndiyo sheria kuu ya barabarani.

Msongamano wa magari

Trafiki 
Basi la Mwendokasi (BRT) jijini Dar es Salaam.

Msongamano wa magari ni hali inayotokea wakati kuna magari mengi barabarani na kufanya mwendo wa magari kuwa wa polepole au kukoma. Majiji makubwa kama vile Nairobi na Dar es Salaam huathirika na hali hiyo hasa nyakati za asubuhi na jioni. Hali hii huathiri sana uchumi. Jiji la Dar es Salaam limejaribu kusuluhisha tatizo hili kwa kujenga mfumo wa mabasi ya mwendokasi.

Tanbihi

Trafiki  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Trafiki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Trafiki MatumiziTrafiki Sheria za trafikiTrafiki Msongamano wa magariTrafiki TanbihiTrafikiAskariBarabaraBasiIdadiJinaLoriMiguuMotokaaMtandaoNjiaTovutiUsafiri

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Dar es SalaamHarusiLugha ya taifaKrismaNgiriMaambukizi ya njia za mkojoKibodiKilwa KivinjeWajitaSamakiItifakiMalaikaKondomu ya kikeMalawiMethaliOrodha ya maziwa ya TanzaniaKuhani mkuuAsiliHifadhi ya mazingiraLughaMajina ya Yesu katika Agano JipyaKalendaKanisa KatolikiHektariTashihisiMuundo wa inshaMatamshiMvuaPunyetoJulius NyerereNdegeEkaristiUfufuko wa YesuSumakuKisasiliFid QHaitiIsraelKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaMadiniMeliFaraja KottaMapafuKitabu cha ZaburiGhanaMjombaUtenzi wa inkishafiJustin BieberUti wa mgongoOrodha ya Watakatifu WakristoNominoHadhiraNembo ya TanzaniaArudhiMtakatifu PauloKonsonantiHifadhi ya SerengetiBahari ya HindiAdolf HitlerHistoria ya EthiopiaNabii IsayaShereheMkwawaUchimbaji wa madini nchini TanzaniaKiswahiliBaraJinaBendera ya KenyaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaAfande SeleWagogoUmoja wa AfrikaMwanamkeMikoa ya TanzaniaMadawa ya kulevya🡆 More