Rozari (kutoka Kilatini rosarium, yaani taji la mawaridi), ni ushanga uliotengenezwa kwanza na Wakatoliki wa Karne za Kati ili kusali kwa kukariri Salamu Maria kadhaa pamoja na kutafakari mafumbo ya imani.
Shanga zilitumika kama pambo tangu kale: barani Afrika zimepatikana za miaka 10,000 KK.
Lini na wapi zilianza kutumika kwa ajili ya sala haijulikani, lakini kuna sanamu ya karne ya 3 KK inayomuonyesha Mhindu akiwa na ushanga wa sala.
Lengo ni kutunza hesabu ya kauli ambazo zinakaririwa kwa kupitisha vidole viwili juu ya punje zilizounganishwa katika kamba au uzi.
Wakristo wa karne ya 15 waliotamani kusali kama watawa Zaburi 150, lakini hawakujua Kilatini au kusoma kabisa, walijifunza kwa urahisi kukariri Salamu Maria 150 huku wakitafakari mafumbo ya maisha ya Yesu, kama alivyowahi kufanya Dominiko wa Prussia (1382-1460), mmonaki Mkartusi.
Lakini shirika lililojihusisha zaidi na Rozari ni lile la Wadominiko.
Mwaka 1569, Papa Pius V aliyekuwa wa shirika hilo, alipitisha sala hiyo kwa Kanisa lote, akapanga mgawanyo wa mafumbo 15 na kukabidhi uenezi wake kwa Wadominiko wenzake.
Mafumbo hayo yaligawiwa katika makundi matatu: 5 ya furaha (utoto wa Yesu), 5 ya uchungu (mateso ya Yesu) na 5 ya utukufu (ufufuko wa Yesu na yatokanayo). Kila fumbo lina Salamu Maria 10, zikitanguliwa na Baba Yetu na kumalizika kwa Atukuzwe.
Mwaka 2002 Papa Yohane Paulo II alipendekeza kuongeza mafumbo 5 ya mwanga ili kuziba pengo kuhusu miaka ya utume wa Yesu.
Mbali na hao, Mapapa wote walihimiza sala hiyo kama njia rahisi kwa wote ya kukumbuka na kuheshimu kazi ya wokovu iliyofanywa na Yesu Kristo.
Sala hiyo imeenea katika baadhi ya madhehebu mengine ya Ukristo, hasa Anglikana.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rozari kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Rozari, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.