Puntland (kwa Kisomali: Dowladda Puntland ee Soomaaliya, Dola la Puntland katika Somalia) ni jimbo la kujitegema la Somalia.
Jimbo hili liko kwenye Somalia kaskazini-mashariki liko kamili kwenye ncha ya Pembe la Afrika.
Jina linatokana na nchi ya Punt ya Kale inayotajwa katika maandiko ya Misri ya Kale. Hadi leo haijulikani jina hili linataja kweli sehemu gani, lakini wataalamu wengi huamini ilikuwa mahali fulani kwenye pwani ya Somalia.
Baada ya kuporomoka kwa Somalia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1991 viongozi wa eneo hili walijitangaza kuwa jimbo la kujitawala. Tofauti na jirani yake Somaliland iliyotangaza uhuru wake, Puntland ilijipa katiba kama jimbo ndani ya Somalia ingawa hali halisi inajitawala tu.
Kwa jumla Puntand ilifaulu kutunza amani na kuepuka kushirikishwa katika vita ndani ya Somalia upande wa kusini.
Sehemu ya magharibi inayoitwa Sanaag inadaiwa pia na Somaliland kwa sababu sehemu hii iliwahi kuwa ndani ya Somalia ya Kiingereza wakati wa ukoloni, lakini wakazi waliamua kujiunga na Puntland.
Idadi ya wakazi ni 4,284,633 kufuatana na kadirio la mwaka 2015.
Lugha rasmi za serikali ni Kisomalia, Kiarabu na Kiingereza.
Wakazi wote ni Waislamu Wasunni. Uislamu ulitangazwa katika katiba kuwa dini rasmi na dini pekee linalokubaliwa.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Puntland, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.