Mkataba wa Versailles ulikuwa mapatano ya kimataifa ya kumaliza Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918) upande wa Ujerumani.
Mapatano yote yalifikiwa kati ya mataifa washindi pekee na serikali ya Ujerumani ilipaswa kuikubali mwishowe. Ujerumani ikatia sahihi kwa malalamiko lakini ilitishiwa ya kwamba wanajeshi wa washindi wangeingia Ujerumani.
Nchi shiriki za mkataba zilikuwa pamoja na Ujerumani hasa Uingereza, Ufaransa na Marekani zilizoitwa "Watatu wakubwa" pamoja na Italia na Japani.
Nchi nyengine upande wa washindi waliotia sahihi lakini hazikuwa na athira katika mapatano yalikuwa Ubelgiji, Bolivia, Brazil, China, Kuba, Ekuador, Ugiriki, Guatemala, Haiti, Ufalme wa Hijaz (Uarabuni), Honduras, Liberia, Nikaragua, Panama, Peru, Poland, Ureno, Romania, Ufalme wa Yugoslavia, Uthai, Chekoslovakia na Uruguay.
Mashariti ya mkataba yalikuwa makali. Ujerumani ilipaswa kukubali ya kwamba ilikuwa na kosa lote kwa vita na kuwa inadaiwa kulipa fidia kwa washindi.
Masharti mengi yalihusu maeneo yaliyotengwa na Ujerumani na kuhamishwa kwa nchi jirani, viwango vya juu kwa jeshi la Ujerumani na madai ya malipo kwa nchi washindi.
Kwa jumla Ufaransa ililenga kuwapa Wajerumani masharti makali sana; Waingereza walitaka kuwa na Ujerumani yenye nguvu ya kiuchumi lakini bila uwezo wa kijeshi; Marekani ilitaka amani ya kudumu.
Ujerumani ilipaswa kupunguza jeshi lake hadi idadi ya wanajeshi 100,000, kubomoa manowari kubwa na kufuta nyambizi zake zote. Eropleni za kijeshi zilikuwa marufuku kwa Ujerumani.
Ujerumani ilipaswa kukubali kulipa fidia kubwa kwa hasara zilizotokea kwa nchi washindi kutokana na vita. Kiwango cha fidia hii kilipangwa kuwa Mark bilioni 132 zilizotakiwa kulipwa hadi 1984.
Wataalamu wengi huona ya kwamba masharti haya makali yalikuwa sababu kuu ya matatizo ya kiuchumi ya Ujerumani yaliyosababisha hali ya kisiasa na kijamii iliyoleta ushindi wa chama cha NSDAP cha Adolf Hitler baada ya 1930.
Sehemu ya mkataba iliunda Shirikisho la Mataifa lililotakiwa kuzia vita zijazo.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkataba wa Versailles, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.