Leo Tolstoy

Lev Nikolayevich Tolstoy (kwa Kirusi Лев Николаевич Толстой; 9 Septemba 1828 - 20 Novemba 1910) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Urusi.

Leo Tolstoy
Leo Tolstoy alivyochorwa na Ilya Efimovich Repin (1844-1930) mwaka 1887.

Huhesabiwa kati ya wanariwaya bora wa fasihi duniani. Kati ya masimulizi yake makuu kuna Vita na Amani pamoja na Anna Karenina.

Familia na urithi

Tolstoy alizaliwa katika familia ya makabaila kwenye kijiji cha Yasnaya Polyana karibu na mji wa Tula. Familia yake ilikuwa na undugu na makabaila wengi na Aleksander Pushkin alikuwa binamu yake.

Mapema Tolstoy alibaki yatima kutokana na kifo cha wazazi wake, akalelewa na dada yake mkubwa.

Alianza kusoma lugha za Kiasia halafu sheria, lakini alipofikia umri wa miaka 20 aliacha masomo akaenda kuishi kwenye mashamba ya familia yake. Hapo alijikuta kama bwana wa familia za wakulima maskini aliokuwa amewarithi kama sehemu ya mali yake, wakiwa kama nusu watumwa jinsi ilivyokuwa kawaida kwa wakulima wengi wa Urusi wa siku zile, kumbe akajitahidi kuboresha maisha yao.

Mwanajeshi, mpenda amani, mla mboga

Kama mwanajeshi alishiriki katika vita vya Urusi kwenye Kaukazi na vita vya Krimea.

Alirudi kwake kama adui wa vita akaendelea kulaumu vita na mabavu kati ya watu akijenga imani yake kwenye mfano wa Yesu Kristo.

Imani hiyo ilileta baadaye ugomvi na Kanisa rasmi la Urusi (Waorthodoksi) lililotumia imani ya Ukristo kwa kubariki jeshi la taifa, wakati Tolstoy alikataa kushiriki vita tena.

Aliendelea kukataa kila aina ya kuua, kwa hiyo alikataa kuchinja wanyama na kula nyama. Aliandika:

      Kula nyama ni mabaki ya unyama ndani ya binadamu. Ulaji mboga ni hatua ya kwanza kwenye njia ya mwangaza.
      Ni hatua moja tu kutoka uuaji wa wanyama kwenda uuaji wa binadamu, vilevile kutoka kutesa wanyama kwenda kutesa watu.
      Kama huwezi kuua watu - vizuri! Kama huwezi kuua mifugo au ndege - bora; wala samaki wala wadudu - bora tena! Ujitahidi kusogea mbele, usipoteze muda kutafakari ni nini inayowezekana au haiwezekani. Fanya unachoweza.

Ndoa na kazi ya fasihi

Mwaka 1862 alimwoa Sofia Andreevna Bers akazaa naye watoto 13.

Kutokana na vitabu vyake juu ya vita vya Krimea alikuwa maarufu nchini Urusi na riwaya kubwa zilizofuata zilijenga sifa zake za kimataifa.

Pamoja na riwaya aliandika pia juu ya dini. Kitabu "Ufalme wa Mungu umo ndani yenu" kiliathiri watu wengi, wakiwa pamoja na Mahatma Gandhi na Martin Luther King.

Mwaka 1910 alikufa kutokana na kifua kikuu akiwa na umri wa miaka 82.

Leo Tolstoy  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Leo Tolstoy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

1828191020 Novemba9 SeptembaKirusiMwandishiUrusi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UkongaUfugajiMahakama ya TanzaniaTungo kishaziSimba S.C.AntibiotikiMagonjwa ya kukuKinyereziKitunda (Ilala)Magonjwa ya machoMazingiraStafeliFasihi andishiMkonoKumaMaambukizi nyemeleziOrodha ya kampuni za TanzaniaWhatsAppHuduma ya kwanzaKiburiVokaliMkoa wa SimiyuUfugaji wa kukuMkoa wa ArushaAzam F.C.FamiliaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMarie AntoinetteBaruaOrodha ya Marais wa ZanzibarHistoria ya WasanguAbedi Amani KarumeWakaguruMillard AyoShambaMmeaAli KibaKassim MajaliwaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaAlgorithimu uchanguajiKitomeoDodoma MakuluMfumo wa uendeshajiMkoa wa KigomaMkopo (fedha)NandyOrodha ya mito nchini TanzaniaKiingerezaMoscowNdovuZuhuraSinzaNamba tasaMadhara ya kuvuta sigaraKisimaGoba (Ubungo)Kiambishi tamatiUNICEFMvua ya maweMuungano wa Tanganyika na ZanzibarOrodha ya Marais wa TanzaniaBibi Titi MohammedHaki za watotoWanyama wa nyumbaniBunge la TanzaniaMkoa wa KilimanjaroTenziLenziEverest (mlima)Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaMwanzo🡆 More