Hiroshima ndio mji mkuu wa Mkoa wa Hiroshima.
Hiroshima | |||
| |||
Nchi | Japani | ||
---|---|---|---|
Kanda | Chūgoku | ||
Mkoa | Hiroshima | ||
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 1,169,018 | ||
Tovuti: www.city.hiroshima.jp |
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2009, mji huo una wakazi wapatao milioni 1.2.
Mji umekuwa maarufu sana duniani kwa sababu ulikuwa mji wa kwanza katika historia kushambuliwa kwa bomu la nyuklia. Tarehe 6 Agosti 1945 ndege ya kivita ya Marekani ilitupa bomu moja lililoua watu 75,000 mara moja na takriban 60,000 wengine walikufa baadaye kutokana na mnururisho wa kinyuklia. Wengine waliendelea kufa kwa sababu ya kansa iliyosababishwa na mnururisho.
Mji ukajengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Jengo la "Kuba ya Bomu ya nyuklia" ni ghofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko. Imeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hiroshima kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hiroshima, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.