HMS Royal Oak ilikuwa manowari iliyotengenezwa nchini Uingereza kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Ilikamilika mnamo mwaka 1916 na kutumika mara baada ya kukamilika katika mapigano ya Jutland dhidi ya manowari za Ujerumani.
Baada ya vita iliona matengenezo kadhaa yaliyolenga kuboresha uwezo wake lakini ilishindikana kuongeza kasi yake kwa hiyo haikufaa tena kwa matumizi ya mapigano wakati wa vita ya pili ya Dunia.
Mnamo 14 Oktoba 1939 HMS Royal Oak ilizamishwa wakati ilikaa katika hori ya Scapa Flow huko Orkney upande wa kaskazini wa Uskoti. Ilishambuliwa na nyambizi ya Ujerumani iliyojulikana kama U-47. Katika usiku ule walifariki wanamaji 835. Kuzama kwa meli hiyo kuliipa wakati mgumu Uingereza na washirika wake katika vita na kwa kufanya hivyo kulipunguza idadi ya meli za kivita za Uingereza na kuleta madhara ambayo yalionekana wakati wa vita. Kuzama kwa meli hiyo kulileta faida kwa kamanda wa kijerumani kutoka katika ile nyambizi ambaye aiitwa Günther Prien, na kutunukiwa cheo cha Knight's Cross of the Iron Cross, na kumfanya kuwa kamanda wa kwanza kutunukiwa cheo hicho katika jeshi la Ujerumani. Kabla ya kuzama kwa meli hii Uingereza haikuwahi kufikiria kuwa meli zao zingeweza kuzamishwa katika hori ya Scapa Flow kwa kushambuliwa na nyambizi, lakini hii ilionesha kuwa Ujerumani ilikua na uwezo wa kuleta mashambulizi karibu zaidi na Uingereza. Baada ya kushtushwa na hilo , Waingereza waliamua kujenga vizuizi katika Scapa Flow ambavyo waliviita Churchill Barriers.
Mabaki ya manowari hiyo bado yanapatikana katika maji ya hori yakitunzwa kama kumbukumbu ya vita na kaburi la wanamaji waliokufa ndani yake na kubaki mle .
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article HMS Royal Oak (08), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.