Mizani ni kundinyota la zodiaki inayojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Libra.
Ni moja ya makundinyota yanayotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia
Nyota za Mizani huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Mizani" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.
Mizani ilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku. Neno Mizano linatokana na Kiarabu ميزان miizaan ambalo linamaanisha "mizani". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Waroma wa Kale waliosema Libra ("mizani"). Kati ya mataifa ya kale mara nyingi nyota za Mizani zilihesabiwa kuwa sehemu ya Akarabu (nge), pamoja na kuangaliwa kama kundi la pekee. Ptolemaio alitumia jina la Χηλαι khelai inayomaanisha "magando" yaani magando ya nge lakini aliiorodhesha kama kundinyota la pekee. Hii ni pia sababu ya kwamba nyota mbili abngavu zaidi bado zinaitwa "Zubani" yaani magando ya nge.
Mizani lipo angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Nadhifa (Virgo) upande wa magharibi na Akarabu (Scorpio) upande wa mashariki.
Mizani huwa na nyota 83 zinazoonekana kwa macho matupu zikiwa na mwangaza unaoonekana wa zaidi ya 6.5 mag.
Nyota angavu zaidi ni Zubani Shimali (Beta Librae au Zubeneschemali) . Ina mwangaza unaoonekana wa mag 2.61 ikiwa na umbali wake unakadiriwa kuwa miakanuru 120 kutoka Dunia. Inafuatwa kwa mwangaza na Zubani Junubi. Majina haya yanamaanisha "Koleo ya Kaskazini na ya Kusini", kwa sababu nyota hizi mbili zilitazamiwa zamani pia kuwa sehemu ya kundinyota jirani ya Saratani, ambako yalimaanisha koleo za "saratani" au kaa.
Jina la (Bayer) | Namba ya Flamsteed | Jina (Ukia) | Mwangaza unaoonekana | Umbali (miakanuru) | Aina ya spektra |
---|---|---|---|---|---|
β | 27 | Zubeneschemali (Zubani Shimali) | 2,61m | 120 | B8 V |
α2 | 9 | Zubenelgenubi (Zubani Junubi) | 2,75m | 77 | A3 |
σ | 20 | 3,29m | 292 | M3 III | |
υ | 3,60m | ||||
θ | 39 | 3,6m | 120 | K4 III | |
τ | 40 | 3,66m | 400 | B3 V | |
γ | 38 | 3,91m | 152 | G8 IV | |
Makundinyota ya Zodiaki Majina ya kisasa yanafuatwa kwa mabano na jina la mabaharia na jina la Kilatini (la kimataifa) | ||
---|---|---|
Kaa (Saratani – Cancer ) • Kondoo (Hamali – Aries ) • Mapacha (Jauza – Gemini ) • Mashuke (Nadhifa – Virgo ) • Mbuzi (Jadi – Capricornus ) • Mizani – Libra ) • Mshale (Kausi – Sagittarius ) • Ndoo (Dalu – Aquarius ) • Nge (Akarabu – Scorpius ) • Ng'ombe (Tauri – Taurus ) • Samaki (Hutu – Pisces ) • Simba (Asadi – Leo ) |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mizani (kundinyota), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.