Waraka wa kwanza wa Petro ni kati ya vitabu 27 vinavyounda Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mtume Paulo alipokaribia kumaliza kazi yake, wengine kati ya mitume na wanafunzi wao walianza kuandika kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Mmojawao ni Mtume Petro, kwa msaada wa Sila, akiwa Roma karibu na kuuawa katika dhuluma ya Kaisari Nero dhidi ya Wakristo (mwaka 64 hivi).
Baada ya kufanya utume huko Antiokia, na kabla ya kupitia Korintho kwenda Roma, aliweza kwa urahisi kutembelea mikoa ya Uturuki Kaskazini wa leo.
Wakristo wa huko ndio walioandikiwa barua hii yenye mafundisho na ibada kuhusu ubatizo na Pasaka.
Pamoja na hayo walihimizwa wasiogope maneno ya watu wengine wasiopendezwa na uongofu wao: hali ngumu ni fursa ya kulingana zaidi na Yesu mpole na mteswa (1Pet 1:1-12; 2:19-25; 3:13-5:14).
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa kwanza wa Petro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Waraka wa kwanza wa Petro, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.